News Mgombea wa ubunge jimbo la Wanging’ombe aahidi kuvutia wawekezaji...

Mgombea wa ubunge jimbo la Wanging’ombe aahidi kuvutia wawekezaji ujenzi wa vyuo

-

Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Njombe. Mgombea ubunge wa jimbo la Wanging’ombe kupitia CCM Dkt. Festo Dugange ameahidi kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakilisha anaweka mazingira mazuri ya wawekezaji kujenga vyuo katika jimbo hilo.

Hayo ameyasema kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Wangingombe uliofanyika kata ya Wanging’ombe kijiji cha Wanging’ombe wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.

Alisema iwapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo atavutia wawekezaji wa serikali na hata binafsi ili waweze kujenga vyuo katika jimbo hilo ili kuongeza tija kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na cha sita.

Alisema chuo hicho kitakapojengwa kitatoa nafasi kwa wanafunzi kujiendeleza katika fani mbali mbali ili waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia katika kuendesha shughuli zao za kimaisha.

Alisema chuo hicho pia kitawawezesha wananchi wote hasa vijana ambao watakuwa tayari kufanya biashara waweze kufanya hivyo ili nao waongeze kipato chao na cha familia kwa ujumla.

“Tukifanya hivyo tutawezesha halmashauri ya Wanging’ombe kupatamapato ya kuhudumia jimbo letu hii kutokana na muingiliano wa watu utakavyokuwa baada ya kujengwa kwa vyuo” Alisema Dkt. Dugange.

Nae mwenyekiti wa CCM wilaya ya Wanging’ombe Stephano Kinyangazi alisema jimbo hilo limepewa heshima kubwa ya kutoa viongozi wa kitaifa  hivyo  wananchi wanapaswa kujivunia na kuiendeleza kwa kuchagua viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi.

“Makamu mwenyekiti, naibu katibu mkuu na katibu wa itikadi na uenezi ngazi ya taifa wote wanatoka Wanging’ombe hivyo tusiwaangushe hawa vingozi tuchague diwani, mbunge na raisi kutoka CCM” Alisema Kinyangazi.

Wananchi walioshiriki kwenye uzinduzi wa kampeni  akiwemo Rehema Ngoda na Elias Mwanzela walisema endapo kutajengwa vyuo katika jimbo la Wanging’ombe  itakuwa faraja kwao kwani watoto wao watakuwa wanasoma karibu tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakienda kusoma vyuo vilivyopo mbali na maeneo yao.

“Namshukuru mgombea kwani jambo la chuo litatukomboa kwenye jimbo la Wanging’ombe kwasababu mpaka sasa hatujawahi kuwa na chuo kinachotambulika kiserikali vipo vyuo vingine tu vya kanisa lakini kwa chuo cha serikali hatuna” Alisema Elias.

“Sisi wakazi wa kata ya Wanging’ombe hatuna chuo hivyo endapo kitajengwa tutafurahi watakuwa watusaidia kwani hali yet ya kiuchumi inatufanya tushindwe kuwapeleka watoto vyuoni kwa kuwa ni gharama kubwa”

 

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

School Reopening: Magoha Responds to Parents on School Fees Payment

Education CS George Magoha on Monday, September 21, assured parents that only tuition fees would be paid once schools...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you