News Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya China

Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya China

-

Polisi wa Macau China wamemkamata Mtanzania waliemtaja kwa jina moja tu la Dossa mwenye umri wa miaka 39 kwa tuhuma za kusafirishwa dawa za kulevya ambapo amekamatiwa kwenye nyumba aliyokua anaishi San Kio Macau akiwa na Dola za Kimarekani, pesa za Hong kong, kilo 15 za dawa aina ya cocaine na kilo nyingine 2.5 za dawa za kulevya ambazo bado hazijafahamika.

Mtandao wa Macau umeripoti kwamba baada ya kumkamata, Msemaji wa Polisi Macau Lei Hon Nei aliitisha kikao maalum na Waandishi wa Habari na kueleza yote, pia wamegundua Dossa alikua amezidisha muda wa kukaa Macau tofauti na ruhusa aliyopewa kwenye VISA.

Vilevile Mamlaka za Macau zimegundua kwamba mzigo uliosafirishwa hivi karibuni kutoka Ulaya kwa kutumia kampuni za usafirishaji hadi Macau mlengwa akiwa Dossa ulikua ni dawa za kulevya aina ya cocaine zinazokadiriwa kuwa na thamani ya USD 413,406 ambazo kwa Tsh. ni zaidi ya MILIONI 900.

Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, Dossa alikiri kununua dawa za kulevya macau kwa Mtu ambae ni Raia wa kigeni na kusema amekua akinunua dawa za kulevya kwa matumizi yake binafsi lakini sio kwa kusafirisha au kuzifanyia biashara, mashitaka dhidi yake tayari yameanza kufanyiwa kazi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Fuel pump/electricity hike: NLC gives update on nationwide protest

The Nigeria Labour Congress (NLC) has...

Reps to commence monthly dialogue with CSOs on assessing MDAs performances

The House of Representatives has announced...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you