News Mwili wa Mama P Funk Majani kuzikwa leo Uholanzi

Mwili wa Mama P Funk Majani kuzikwa leo Uholanzi

-

Mwili wa mama mzazi wa mtayrishaji wa muziki wa BongoFleva P Funk Majani, Aunt Sheilah umeshindikana kurudi ili kuzikwa Tanzania kwa sababu ya changamoto ya usafiri na Ugonjwa wa Corona, hivyo unatarajiwa kuzikwa leo nchini Uholanzi.

Mwenyekiti wa kamati wa maandalizi wa msiba huo ambaye ni msanii Soggydogg Anter, amesema mwili utazikwa Uholanzi na P Funk mwenyewe yupo huko kwa ajili ya mazishi, ambapo  atarejea Tanzania Ijumaa usiku na siku ya Jumamosi watafanya dua maalum kwa marehemu.

“Siku ya leo tunarajia mwili wa mama mzazi wa P Funk Majani Aunt Sheilah kuzikwa nchini Uholanzi, imebidi azikwe huko kwa sababu usafiri ulikuwa mgumu na wenzetu bado wana wasiwasi na ugonjwa wa Corona, P Funk Majani mwenyewe tayari yupo huko kwa ajili ya mazishi na atarejea Tanzania siku ya Ijumaa usiku, kisha Jumamosi itafanyika dua ya marehemu nyumbani kwake Bamaga mahali ambapo ipo studio za Bongo Records” amesema Soggydoggy Anter

Mama wa P Funk Majani alifariki nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu siku ya Septemba 8, na taarifa kuhusu kifo chake zilitoka Tanzania siku ya Septemba 10.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Benki ya CRDB kuipendezesha Tanzania

Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wamezindua kampeni ya utunzaji mazingira kwa kuhamasisha...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you