News Ndege za kivita za Israel zaishambulia Gaza baada ya...

Ndege za kivita za Israel zaishambulia Gaza baada ya roketi za Palestina kurushwa Israel

-

- Advertisment -

Israel imeshambulia eneo la Gaza kwa mabomu mapema leo baada ya mashambulizi ya roketi kutoka ukanda huo kurushwa Israel wakati ambapo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alipokuwa akitia saini makubaliano ya kurejesha uhusiano kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain mjini Washington.


 Karibu roketi mbili zilirushwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza huku moja ikizuiliwa na mfumo wa Israel wa kuzuia mashambulizi.

 Kulingana na maafisa wa huduma za dharura roketi zengine mbili zilianguka katika mji wa Ashdod na kuwajeruhi watu wawili. 

Huko Gaza waandamanaji wameonekana kuyakanyaga na kuyachoma moto mabango yaliyo na picha za viongozi wa Israel, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Ila Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaamini kutiwa saini kwa makubaliano hayo kutaleta amani.”Na baraka za amani ya leo zitakuwa kubwa. 

Kwanza kwasababu amani hii itapanuka na kujumuisha mataifa mengine ya Kiarabu na kufikisha mwisho mgogoro wa Waarabu na Waisraeli.

“Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameonya kuwa mikataba haitoleta amani Mashariki ya Kati hadi pale Israel na Marekani watakapolitambua taifa la Palestina.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Cross River State police commissioner loses mother

Hajia Hajarat Nma Abdulkadir, mother of...

Buhari condoles Umahi, Ebonyi people over death of scores in fatal accident

President Muhammadu Buhari has offered his condolences to the government and people of Ebonyi State over...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you