News Rais Trump anaamini Saudi Arabia itarekebisha uhusiano na Israel

Rais Trump anaamini Saudi Arabia itarekebisha uhusiano na Israel

-

- Advertisment -

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini Saudi Arabia itafuata Bahrain na Falme za Kiarabu (UAE) katika kurekebisha kabisa uhusiano na Israeli.

Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Saudia ni miongoni mwa nchi kadhaa ambazo anaamini ziko katika hatihati ya kufungua uhusiano wa kidiplomasia na Tel Aviv, akisema kwamba baada ya kuzungumza na Mfalme Salman, anafikiria nchi hiyo itafanya hivyo “kwa wakati unaofaa.”

“Tuna nchi nyingine nyingi ambazo zitajiunga nasi, na watajiunga nasi hivi karibuni,” Trump alisema saa chache baada ya Bahrain na UAE kutia saini rasmi hati za kurekebisha uhusiano na Israeli.

“Tutakuwa na nchi 7 au 8 au 9. Tutakuwa na nchi zingine nyingi zitakazojiunga nasi, zikiwemo nchi kubwa” alisema Trump.

Wakati wa hafla rasmi ya kutiwa saini Jumanne, Trump alisema makubaliano hayo yataimaliza “miongo kadhaa ya mgawanyiko na mizozo” katika eneo hilo na kuleta “mwazo wa Mashariki ya Kati mpya.”

“Shukrani kwa ujasiri wa viongozi wa nchi hizi tatu, tunachukua hatua kubwa kuelekea siku za usoni ambapo watu wa dini zote na asili zote wataishi pamoja kwa amani na ustawi,” Trump alisema, akihutubia mamia ya wageni waliokusanyika katika hafla hiyo Ikulu.

Bahrain imekuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli Ijumaa iliyopita baada ya Misri mnamo 1979, Jordan mnamo 1994 na UAE mnamo mwezi Agosti.

Mbali na makubaliano ya nchi mbili yaliyosainiwa kati ya Israeli na mataifa ya Kiarabu, nchi hizo tatu zimetia saini makubaliano ya “Abraham Accords” na nchi ya Marekani.

Waziri wa Mambo ya nje wa Bahrain Abdullatif bin Rashid Alzayani ameelezea makubaliano hayo kama “hatua muhimu ya kwanza” kuelekea kuanzisha amani zaidi katika eneo hilo.

“Sasa ni jukumu letu kufanya kazi haraka na kwa bidii kuleta amani na usalama wa kudumu ambao watu wetu wanastahili. Suluhisho la haki, pana na la kudumu la serikali mbili kwa mzozo wa Palestina na Israeli litakuwa msingi wa amani” alisema Alzayani.

Makubaliano hayo yameshambuliwa na Palestina na kwamba hayana faida yoyote kwa taifa hilo na yanapuuza haki zao.

Mamlaka ya Palestina yameisema makubaliano yoyote na Israeli yanapaswa kutegemea Mpango wa Amani wa Kiarabu wa 2002 juu ya kanuni ya “ardhi kwa amani” na sio “amani kwa amani” kama Israeli inavyodumisha.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

UN: Yemeni belligerents launch prisoner swap talks

A meeting between the Yemeni government and Houthi rebels on swapping prisoners and detainees have started in Geneva, the...

Lavrov says Russia is ready to mediate in the Gulf crisis

Russian Foreign Minister Sergey Lavrov announced today that his country is willing to mediate in the crisis between Qatar...

How the Expressway will affect property owners along its path

 Several property owners along Nairobi’s Mombasa Road face eviction as the government moves in to construct the Nairobi Expressway...

Victory for Badi team as court reverses order on NMS

 A judge has reversed her orders on the creation of the Nairobi Metropolitan Services in a decision which is...

Amina Mohamed gets nod to proceed to next round in WTO race

 Kenya's candidate in the race for World Trade Organisation (WTO) Director-General post CS Amina Mohamed has qualified for the...

Covid-19: Kenya records 148 new cases, tally rises to 36,724

 Kenya has recorded 148 more Covid-19 positive cases in the past 24 hours raising the country's total caseload to...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you