News Shujaa' wa filamu ya Hoteli Rwanda atapewa haki kisheria,...

Shujaa' wa filamu ya Hoteli Rwanda atapewa haki kisheria, yasema Rwanda

-

- Advertisment -

Msemaji wa uendeshaji mashitaka wa umma nchini Rwanda ameihakikishia familia kuwa ‘‘shujaa’’ wa filamu ya Hoteli Rwanda na mpinzani wa nchini hiyo Paul Rusesabagina atapata haki ya kisheria katika kesi dhidi yake inayoendelea.

‘’Hata alipokamatwa ilitangazwa wazi…alipouguwa alipata huduma ya matibabu, alipewa jopo la mawakili tena bure… Kesi itakuwa wazi kwa umma.’’ Amesemamsemaji wa ofisi yauendeshaji mashitaka ya umma nchini Rwanda Paul Nkusi katika mahojiano na kipindi cha BBC Newsday

Bwana Nkusi amesema, la muhimu ni kwamba alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Rwanda na sasa yuko mikononi mwa polisi ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili.

Bwana Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya raia, kuwajeruhi raia, kupora na kuharibu mali za raia, kuunda kundi lenye silaha hususan ni FNL ambalo linawatumikisha watoto vitani, na kuhusika katika shuguli za ugaidi, amesema Bwana Nkusi.

Nkusi amesema Rusesabagina binafsi alithibitisha mwenyewe kuhusika katika baadhi ya vitendo hivi.

‘’Ninaweza kutaja baadhi ya ushahidi aliousema mwenyewe…alisema alituma pesa kwa njia ya Western Union na kukusanya pesa za kuunga mkono kikundi cha FNL’’, Alisema Bwana Nkusi.

Familia ya Rusesababigina ambaye alipata umaarufu baada ya kucheza filamu ya Hoteli Rwanda juu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, inasema kuwa alitekwa nyara alipokuwa safarini Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu.

Msemaji huyo wa Ofisi ya mwendesha mashitaka ya umma amesema kuwa kwasasa anashikiliwa katika kituo cha polisi Remera na mawakili wake wanamtembelea.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

UN: Yemeni belligerents launch prisoner swap talks

A meeting between the Yemeni government and Houthi rebels on swapping prisoners and detainees have started in Geneva, the...

Lavrov says Russia is ready to mediate in the Gulf crisis

Russian Foreign Minister Sergey Lavrov announced today that his country is willing to mediate in the crisis between Qatar...

How the Expressway will affect property owners along its path

 Several property owners along Nairobi’s Mombasa Road face eviction as the government moves in to construct the Nairobi Expressway...

Victory for Badi team as court reverses order on NMS

 A judge has reversed her orders on the creation of the Nairobi Metropolitan Services in a decision which is...

Amina Mohamed gets nod to proceed to next round in WTO race

 Kenya's candidate in the race for World Trade Organisation (WTO) Director-General post CS Amina Mohamed has qualified for the...

Covid-19: Kenya records 148 new cases, tally rises to 36,724

 Kenya has recorded 148 more Covid-19 positive cases in the past 24 hours raising the country's total caseload to...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you