News Trump kutembelea maeneo yaliathiriwa na moto Califonia

Trump kutembelea maeneo yaliathiriwa na moto Califonia

-

- Advertisment -

Rais Donald Trump wa Marekani amesema atakutana na kitengo cha huduma za dharura cha California hapo kesho katika kipindi hiki ambacho rekodi za janga la moto zinaonesha kuwauwa watu 27 katika eneo la Pwani ya Magharibi ya taifa hilo.

Pamoja na athari zilizopo sasa lakini bado maafisa wanaonyesha uwezekano wa kutokea maafa zaidi wakati moto huo ukitapakaa katika maeneo ya California, Oregon na Washington ambayo kwa sasa yametenganishwa na moto mkubwa, uliochochewa na hali ya ukame.

Mpinzani wa Trump katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, Joe Biden anaunganisha janga hilo la moto na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Trump anatarajiwa kukutana na wakuu wa huduma za dharura wa California, ambao wanapambana na moto ulioteketeza zaidi ya ekari milioni 3.2 katika jimbo hilo mwaka huu pekee.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Makamu wa Rais atangaza neema kwa wakulima wa Mahindi wilayani Ludewa

 Na Amiri Kilagalila,NjombeSerikali imetangaza kuanzishwa kwa kituo cha kununua mazao ya mahindi wilayani Ludewa mkoani Njombe,kutokana na changamoto kubwa...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you