News Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umerudi tena...

Umoja wa Mataifa wasema ukosefu wa chakula umerudi tena Yemen

-

 

Mkuu wa misaada ya kiutu katika Umoja wa Mataifa ameonya kwamba uhaba wa chakula umerudi tena katika nchi iliyozongwa na machafuko ya Yemen. 

Mark Lowcock amezitaja Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Kuwait kama nchi ambazo hazijatoa msaada wowote katika kiasi cha dola bilioni 3.4 zinazohitajika mwaka huu. 

Lowcock amesema Umoja wa Mataifa ulilimaliza tatizo hilo nchini Yemen mwaka jana kwa kuwa wafadhili walitoa haraka michango iliyofikia asilimia 90 ya kiwango jumla kilichoombwa. 

Mkuu huyo amesema maisha ya mamilioni ya watu yaliokolewa kwasababu misaada iliongezwa. 

Ila kwa sasa anadai kwamba ni asilimia 30 tu ya kiasi cha pesa kilichoitishwa ambacho kimetolewa na kwamba Wayemen milioni tisa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula, maji na matibabu.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Akeredolu’s son threatens to sue Deputy Gov over false accusation

The son of Governor Oluwarotimi Akeredolu...

Poll: Biden Leads Trump in Wisconsin; Pennsylvania A Tight Race

- Other Media news - In Wisconsin, Biden leads with 48 percent support, while Trump trails with 43...

Barbara wa Simba afanya makubaliano na timu ya AL Ahly ya Misri

Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez akiongozana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi wametembelea makao makuu ya klabu...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you