News VIDEO: NEC yawarejesha wagombea udiwani 47 waliowekewa pingamizi

VIDEO: NEC yawarejesha wagombea udiwani 47 waliowekewa pingamizi

-

- Advertisment -

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezipitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 87za wagombea udiwani na kuwarejesha wagombea 47 wa udiwani na kuwarejesha wagombea udiwani katika orodha ya wagombea udiwani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera Charles wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kikao cha Tume kilichokaa jana jijini Dar es Salaam.

Dkt. Charles ametaja kata ambazo wagombea wake wamerejeshwa kuwa ni kata ya Mwanhuzi (Meatu), Kondoa Mjini (Kondoa Mjini) Msasa (Handeni Mjini), Bunju (Kawe), Bunju (Kawe), Ipagala (Dodoma Mjini), Isuto (Mbeya Vijijini), Iwiji (Mbeya Vijijini), Kichangani (Morogoro Mjini), Kimara (Ubungo).

Ametaja kata nyingine kuwa ni kata ya Likongowele (Liwale), Matumbulu (Dodoma Mjini), Nsalala (Mbeya Vijijini), Ulenje (Mbeya Vijijini), Muriti (Ukerewe), Ruvu (Same Magharibi), Kisutu (Bagamoyo), Majimaji (Tunduru), Mtibwa (Mvomero), Unyianga (Singida Mjini) na Kagondo (Bukoba Mjini).

Wagombea wengine waliorejeshwa ni kutokea kwenye kata ya Kaloleni (Moshi Mjini), Mlabani (Kilombero), Fukayosi (Bagamoyo), Igurwa (Karagwe), Kauzeni (Morogoro Mjini), Maisaka (Babati Mjini), Ndama (Karagwe) Olorien/Magaiduru (Ngorongoro), Kilole (Lushoto), Ngwelo (Lushoto), Hondomairo (Kondoa Mjini), Nyasiura (Bunda Mjini), Ikhanoda (Singida Kaskazini), Nyabiyonza (Karagwe), Kibiti (Kibiti), Ruvu Remit (Simanjiro), Ihanda (Karagwe), Mabanda (Handeni Mjini), Bungu (Kibiti), Kapala Msenga (Mpanda Vijijini), Businde (Kyerwa), Igoma (Mbeya Vijijini), Likongowele (Liwale), Shizuvi (Mbeya Vijijini), Mlembwe (Liwale) na Tambukareli (Dodoma Mjini).

Katika hatua nyingine, Dkt. Charles amesema Tume pia imekataa rufaa 30 za wagombea udiwani ambao hawakuteuliwa kutoka kwenye kata za Tongwe (Muheza) Kiomboi (Iramba Magharibi), Jangwani (Ilala), Mlali (Mvomero), Kiloleni (Sikonge), Mbasa (Kilombero), Dakawa (Mvomero),

“Kata nyingine ni Dakawa (Mvomero), Jibondo (Mafia), Kigombe (Muheza), Buhumbi (Magu), Mlali (Mvomero), Olbalbal (Ngorongoro), Kidete (Kilosa), Bugene (Karagwe), Kihanga (Karagwe), Mabogini (Moshi Vijijini), Hemtoye (Mlalo), Mlali (Mvomero), Mbaramo (Mlalo), Mbaru (Mlalo), Okaoni (Moshi Vijijini), Nangando (Liwale), Magomeni (Kinondoni), Kitangiri (Ilemela), Dareda (Babati Vijijini), Iganjo (Mbeya Mjini), Ipembe (Singida Mjini), Kilema Kaskazini (Vunjo) na Nyamhongolo (Ilemela)”, amesema Dkt. Charles.

Dkt. Charles ameongeza kuwa, Tume imekataa rufaa 10 za kupinga wagombea udiwani walioteuliwa kutoka kata za Forest (Mbeya Mjini), Mabatini (Mbeya Mjini), Mkowe (Kalambo), Kaloleni (Moshi Mjini), Mwangoi (Mlalo), Malibwi (Lushoto), Kwa Kilosa (Iringa Mjini), Kihesa (Iringa Mjini), Nzubuka (Tabora Kaskazini) na Ihumwa (Dodoma Mjini).

Amesema idadi hiyo inafanya jumla ya rufaa za wagombea Udiwani zilizotolewa uamuzi kufikia 331 na Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku.

Ameongeza kuwa wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.

                     TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI……USISAHAU KUSUBSCRIBE

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

BREAKING: Lagos approves full reopening of churches, mosques

Lagos State Governor, Babajide Sanwo-Olu, has...

Girl Accidentally Exposes Nick Ruto’s Trip to Moi Hotel [PHOTO]

Details have emerged about Nick Ruto's trip to Lake Bogoria Spa Resort on September 5, 2020. In a photo that...

Watu wawili wamefariki katika kimbunga nchini Ugiriki

 Kimbunga ambacho kimetokea nchini Ugiriki kimepelekea vifo vya wawili huku mtu mmoja akiripotiwa kupotea.Mtu huyo  hajulikani  alipo  huku  harakati ...

Barua ya wazi ya Thiago Alcantara kwa Bayern

 Thiago Alcantara, ambaye amesaini mkataba wa miaka minne na Liverpool, anasema kuondoka Bayern Munich ilikuwa "uamuzi mgumu zaidi" katika...

UPDP yazindua kampeni zake rasmi

 Mgombea wa Urais wa Chama cha United Peoples Democratic Party, (UPDP) Twalib Ibrahim Kadege amezindua rasmi kampeni za urais...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you