News Vyama vya siasa vyaaswa kuzingatia sheria za uchaguzi

Vyama vya siasa vyaaswa kuzingatia sheria za uchaguzi

-

- Advertisment -

 

Na Timothy Itembe Mara.

TUME ya Taifa ya uchaguzi NEC  imeviasa vyama vya siasa  vinavyoshiriki uchaguzi mkuu 2020 kuhakikisha wanazingatia masharti yaliyowekwa ikiwemo swala la mda wa kuanza na kumaliza ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tarime vijijini,Apoo Tindwa aliwaambia waandishi wa habari kuwa tume haitamfumbia macho yeyote ataye vunja kanuni na taratibu za uchaguzi kwa sababu sheria iko pale pale haibadiriki. 

“”Nawakumbusha  Wagombea wa Ubunge pamoja na Udiwani kuzingatia maadili na kanuni za uchaguzi  kwa kuzingatia muda wa kuanza kampeni pamoja na muda wa kumaliza lampeni ambapo kuanza ni kuanzia saa 1 asubuhi  hadi saa 12 jioni”alisema Tindwa.

Tindwa aliongeza kusema kuwa kampeni  za uchaguzi kwa mwaka huu  zimekuwa za hamasa kubwa na Watu wamehamasika lakini  vyama  vinavyofanya  kampeni  visifanye kampeni za kichochezi  na kwa  Wagombea watao kiuka tu kanuni Tume haitawafumbia macho.

Akiendelea kuzungumza amesema kuwa Halnashauri ya Vijijini  ina Kata 26 pamoja na vituo 531 vya kupigia kura  na kuingeza kuwa kwa wale waotangaza mikutano ya kampeni mwisho ni saa 2 usimu hairuhusiwi  kuendelea kutangaza hadi eneo linguine na kuwabugudhi Watu wa eneo lingine ambao tangazo haliwahusu .

Kwa upande wa vyombo vya Habari vimetahadhalishwa kutoegemea upande wa Chama kimoja na kutoandika Habari za uchochezi  kwa Mwandishi  atayekiuka asishangae anafikishwa mahara husika  chombo chake kinafungiwa nayeye kufikishwa Nahakamani na kusisitiza atakaye kiuka ajue sheria iko pale pale

Aidha  amesema kuwa Wagombe wa ubunge wako watatu Mwita Mwikwabe Waitara(CCM) John Heche(CHADEMA) Charle Mwera( ACT)  na mgombea  ubunge kupitia chama cha NRA  Stiven Joseph Mirumbe aliwekewa pingamizi kwa kutokidhi vigezo ambapo kwa upande wa udiwa aliwekewa pingamizi Denson John Makanya(CHADEMA)  pamoja na Amos Sagara (CCM) Amos Sagara  baadae pingamizi lake lilifutwa ambapo kwa sasa ni Mgombea Kata ya Sirari,

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Several bandits killed as troops raid Kaduna forest

The Defence Headquarters on Friday said the Air Component of Operation Thunder Strike destroyed bandits’ meeting...

Abia: Ikpeazu has done well – Ngwa Patriots Forum

The president of Apex Ngwa Socio-Political...

French Christian group allegedly backs Syrian regime

A France-based Christian group has allegedly been supporting a militia in Syria loyal to the Bashar al-Assad regime and...

Marekani kupiga marufuku TikTok na WeChat

TikTok na WeChat zitapigwa marufuku nchini Marekani kuanzia Jumapili, endapo Rais Donald Trump atakubali kutekeleza mkataba wa dakika za...

RC Ndikilo atembelea kiwanda cha kisasa cha kuunganishia magari cha GFA Kibaha

 Serikali mkoani Pwani imewataka wawekezaji mbali mbali wa ujenzi wa viwanda kuhakikisha kwamba wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you