News Wanawake Serengeti wadai kura zote kura zote wampa Ruge,...

Wanawake Serengeti wadai kura zote kura zote wampa Ruge, wawaomba wanaume kuwaunga mkono

-

 Na Timothy Itembe Mara.

Wanawake wamesema watamuunga mkono mgombea Ubunge jimbo la Serengeti katika uchaguzi wa 2020 ili kuhakikisha anaenda kuwa Mbunge na kuwawakilisha kwa lengo la kuwalwetea maendeleo.

Wanawake hao wametumia nafasi hiyo kuwaomba wanaume kwa ujumla kuwaunga mkono pindi hiki kwasababu wamekuwa wakiwaunga mkono katika chaguzi zilizopita.

Vaileth Seronga ambae ni mkazi wa Serengeti alisema kuwa zamu hii ni ya kwenda na mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Catherine Ruge(Msubati) ili atuletee maendeleo.

“Tuna hifadhi ya wanyama ndani ya wilaya yetu ya Serengeti lakini ajira zikitoka wanaoajiriwa ni watu kutoka maeneo mengine kwa hali hiyo wanawake tunakuunga mkono mgombea wetu ili ukatutetee na vijana wetu waajiriwe hifadhini, pia ukifanikiwa na kuwa Mbunge tunaomba utuunge mkono vikundi tupate mikopo kwa gharama nafuu”alisema Seronga.

Seronga aliongeza kuwa wanawake wakipatiwa mikopo wa riba ya gharama nafuu wataenda kupata mitaji na kuanzisha biashara ndogondogo zitakazowainua kiuchumi kwa lengo la kuendeshea maisha.

Naye Melisyani Bensoni alitupia lawama halmashauri kwa kuwatoza kodi ya uchafu shilingi alfu 2000 kwa mwezi pasipo kuzingatia kipato walichonacho kuwa ni kidogo.

 Bensoni aliongeza kuwa wamama wauza mboga mtaji wao ni shilingi alfu 2000  na faida ni shilingi alfu moja cha ajabu halmashauri bila kujali kipato wanachopata wanawalipiza na kuwatoza kodi ya uchafu shilingi 2000 bila kuzingatia kipato wanacho kipata kutokana na biashara wanayofanya.

Katika mkutano huo wa kampeni za uchaguzi uliofanyikia viwanja vya majalalani wilayani hapo mgombea ubunge  Chadema Catherine Nyakao Ruge aliwaambia wananchi kuwa akifanikiwa na kuwa Mbunge atahakikisha kuwa analeta maji kwa kuwa maji ni uhai.

Ruge aliongeza kuwa akiwa mbunge atawaboreshea wakazi wa Serengeti huduma za Afya na wagonjwa watapatiwa huduma kwa kuzingatia sheria na sera zilizopo za  Afya sio vinginevyo.

Katika mkutano huo,Teckra Johanes aliwataka wananchi kutofanya kosa badala yake wachague mgombea urais kupitia Chadema,mgombea ubunge jimbo la serengeti,Catherine na wagombea udiwani wote wa Chadema ili kuwaletea wananchi maendeleo na kuondokana na kero zilizopo.

Johanes alimtaka mgombea ubunge huyo kuhakikisha anasimamia ahadi anazo ahidi kwa wananchi pindi atakapofanikiwa na kuwa mbunge wa Serengeti na asije akawaangusha wapiga kura.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Erdogan: Turkey keeps calm despite Greece’s provocation

Turkey keeps a prudent and calm attitude despite Greece’s provocations and rising tension in the region, the Turkish president...

Saudi dissidents form pro-democracy political group

A group of Saudi dissidents, most of them in exile, on Wednesday announced the formation of a party to...

Kogi: FCT Minister reacts to death of 23 persons in Lokoja tanker explosion

The FCT Minister of State, Ramatu Aliyu, has reacted to the Kogi State tanker explosion, which claimed the lives...

Insecurity: CISS faults report on Nigeria’s terrorism index

A recent report which ranked Nigeria...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you