News Watuhumiwa 32 washitakiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha uhalifu

Watuhumiwa 32 washitakiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha uhalifu

-

- Advertisment -

Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yaoImage caption: Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao

Kundi la watu 32 wako mahakamani nchini Rwanda kwa tuhuma za kuwa wapiganaji wa kundi la Rwanda National Congress RNC linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC.

Baadhi yao wanaongozwa na meja mstaafu Wa jeshi la Rwanda,Habib Mudathiru ,wengine wakiwa askari watoro kutoka jeshi la Rwanda.

Wanashitakiwa kujiunga na wapiganaji Wa kundi la RNC ambalo linaongozwa na Jenerali Kayumba Nyamwasa mkuu Wa zamani Wa majeshi ya Rwanda anayeishi uhamishoni nchini Afrika kusini.

Kuna pia wengine waliojiunga na wapiganaji Wa vuguvugu la P5 ambalo pia linaendesha harakati zake mashariki mwa DRC.

Wote walikamatwa katika mapigano mashariki mwa Congo mwaka 2019 na baadae kukabidhiwa Rwanda.

Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao na kusema kwamba waliingizwa katika makundi hayo kwa nguvu. Kesi inaendelea.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Neymar afungiwa game mbili

Staa wa PSG Neymar amefungiwa mechi 2 kutokana na kadi nyekundu aliyooneshwa katika mchezo dhidi ya Marseille mchezo wa...

Diva atangaza rasmi kuacha kazi Clouds FM

 Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva atangaza rasmi kuacha kazi ndani ya kituo hicho.Kupitia...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you