News Yanga kuivaa Mlandenge FC leo

Yanga kuivaa Mlandenge FC leo

-

 

LEO Septemba 16, kikosi cha Yanga kinachonolewa na Zlatko Krmpotic raia wa Serbia kitashuka Uwanja wa Azam Complex kumenyana na Mlandenge FC ya kutoka visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo utapigwa saa 1:00 usiku  una malengo ya kuboresha viwango vya nyota wa Yanga kutokana na kukosa mechi fitness baada ya kutokuwa na muda mrefu wa pre-season kutokana na janga la Virusi vya Corona. 

Yanga ilianza maandalizi ya msimu wa Ligi Kuu Bara Agosti 15 ikiwa na wachezaji11, ambapo ilianza kufanyia mazoezi yake Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam ila kwa sasa imeweka kambi jumla Kigamboni. 

Tayari imeshacheza mechi mbili ndani ya ligi na imeshinda moja mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0 na kuambulia sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons zote Uwanja wa Mkapa. 

Mechi yake inayofuata ni dhidi ya Kagera Sugar,  Septemba 19, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Benki ya CRDB kuipendezesha Tanzania

Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wamezindua kampeni ya utunzaji mazingira kwa kuhamasisha...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you