News ADC waendelea kupeperusha vipaumbele vyao vitatu

ADC waendelea kupeperusha vipaumbele vyao vitatu

-

 

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita Chama cha ADC Queen Sendinga,ameendelea na kampeni zake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na tume ya uchaguzi huku akiendelea kusisitiza vipaumbele vitatu pindi watakapoweza kushika Dola.

Akizungumza na wakazi wa mji wa Njombe katika mkutano wake uliofanyika eno la stendi ya zamani,amesema vipaumbele vyake ni elimu,afya na kilimo huku wakianza na elimu kwa kuwa ni ufunguo wa maisha.

“Vipaumbele vyetu.Cha kwanza elimu,afya na kilimo na tumetanguliza elimu kwa kuwa ni ufunguo wa maisha,kwasababu unapomnyima binadamu elimu unampa umaskini wa akili mwili mpaka roho”Queen Sendinga 

Amesema serikali iliyopo madarakani imekuwa ikitangaza kutoa elimu bure lakini bado katika utekelezaji wa adhma yao umekuwa na changamoto kubwa.”Tunaambiwa elimu ya Tanzania ni bure,hakuna bure hapa tunapigwa changa la macho.Imetolewa ada mashuleni bado kumebaki michango,kumebaki mzigo kwa wazazi kununua vitabu”alisema Queen Sendinga 

Aliongeza kuwa “Chama cha ADC kama tutapata ridhaa ya kuongoza nchi ya Tanzania,kwanza tunakwenda kubadilisha mitaala katika mfumo wetu wa elimu ili mitaala iweze kuwa rafiki”aliongeza Queen Sendinga

 

Kuhusu swala la maji mkoani Njombe amesema “Njombe hapa maji yanatiririka kule kwenye maporomoko wanashindwa kuwa wabunifu kuwapelekea wananchi maji majumbani,na kila uchaguzi wanakuja kuwaomba kura”Queen Sendinga 

Aidha ameendelea kusisitiza swa la amani kuelekea siku ya uchaguzi”Tuna shida sawa lakini bado tuko kwenye amani,uvumilivu huu tuendelee nao na mtunze amani tuliyonayo kwa ghalama yoyote ile ili tuweze kupata mafanikio,tusidanganywe na mtu kuandamana,kushika mawe,kubeba panga kwasababu hakukupi maisha bora zaidi ya kufanya maamuzi kwenye boksi la kura”Queen Sendinga

Naye mwenyikiti wa vijana taifa wa chama hicho amewataka watanzania kufanya mabadiliko kwa kuwa inawezekana kwa kuwa bado nchi ina maadui watatu ambao ni umasikini,maradhi na ujinga.

“Kuna sababu gani ya kukumbatia chama cha mapinduzi wakati watanzania wanakusanyiwa kodi zao na isiwe sehemu ya kuondoa kero na changamoto zinazowakabili ili waweze kupata matibabu,serikali ya ADC ni miongoni mwa vipaumbele vyake vikubwa ni afya ya mtanzania”alisema mwenyekiti wa vijana

Baadhi ya wakazi mjini Njombe waliofika katika mkutano huo wameahidi kwenda kuchagua viongozi watakao wafaa na kulifikisha taifa pale wanapohitaji kimaendeleo.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Wananchi wa Chamwino Ikulu wajitokeza kwa wingi vituoni kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani

Wananchi wa Chamwino Ikulu mkoani Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kituo cha kupigia kura cha Ukumbi wa Kijiji...

Schools Reopening: Magoha Offered Solution on All Students’ Return

Health CS Mutahi Kagwe and his Education counterpart George Magoha have been offered a solution on how to ensure all...

DJ wa Harmonize afunguka mahusiano yake na Linah (+Video)

try{__scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress();}catch(e){setTimeout( function(){ __scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress(); } , 3000 )};DJ wa Harmonize maarufu kama DJSEVE @djsevenworldwide amefunguka mahusiano...

Job Opportunity at Yetu Microfinance Bank PLC, Branch Manager

 Position: Branch Manager Location: Mngeta, Kilombero District Key details Yetu Microfinance Bank...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you