News Afghanistan yaishutumu Taliban kwa kuvuruga amani nchini

Afghanistan yaishutumu Taliban kwa kuvuruga amani nchini

-

 Serikali ya Afghanistan imelishutumu kundi la Taliban kwa kutoa visingizio kuhusu mchakato wa amani na kuendeleza vurugu.

Makamu wa rais wa Afghanistan Sarwar Danish, alihutubia hafla moja aliyohudhuria katika mji mkuu wa Kabul na kusema kuwa Taliban haina sababu yoyote ya kupigana na serikali ya nchi.

Akielezea Taliban kuendeleza harakati zao za kuvuruga amani mjini Kabul hivi karibuni, Danish alisema, ‘‘serikali ya Afghanistan imekuwa mstari wa mbele muda wote ili kudumisha amani nchini, ilhali Taliban imekuwa ikivuruga kwa visingizio.’’

Marekani ilianzisha mazungumzo ya kupunguza vurugu na Taliban mnamo mwezi Desemba 2019, na kuishia kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini tarehe 29 Februari.

Kufuatia hatua hiyo, mchakato wa mazungumzo kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan ukaanzishwa tarehe 12 Septemba katika mji mkuu wa Doha nchini Qatar.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Amnesty: Waandamanaji 12 wauawa Nigeria

Lagos:Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema katika ripoti yake jana kwamba vikosi vya usalama...

Kenyan Vegetable Vendors Make Ksh235M in 3 Days Online

A group of Kenyan vegetable vendors raked in Ksh235 million over the last 3 days in an online virtual...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you