News Ajinyonga baada ya kuzuiliwa kurudi nyumbani usiku

Ajinyonga baada ya kuzuiliwa kurudi nyumbani usiku

-

Mwanafunzi aliyemaliza darasa la 7 wiki iliyopita katika shule ya msingi Njungwa, Kijiji cha  Ngayaki wilayani Gairo, Rahel Yohana (14), amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kanga huku chanzo kikitajwa ni ugomvi kati yake na mama yake mzazi aliyekuwa akimkataza kurudi nyumbani usiku.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 mwaka huu, na akatoa wito kwa wale watu wanaoona njia ya bora ya kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kukatisha uhai wao, kuwa siyo sahihi na badala yake watafute ufumbuzi wa changamoto zao kwa wataalam.

“Aligombezwa na mama yake kwa kosa la kurudi nyumbani mara kwa mara usiku na alitoweka nyumbani na ndipo alipokutwa amejinyoga vichakani, nitoe wito kwa watu ambao wanafikiri ‘shortcuts’ ya changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kuamua kujinyonga, hiyo si sahihi ni bora ukutane na wataalam wa kisaikolojia ili wakusaidie”, amesema Kamanda Mutafungwa.

Na mwili wa mtoto huyo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Melania Trump pulls out of campaign rally due to Covid cough

Melania Trump has decided against accompanying US President Donald Trump to a campaign rally because of a lingering cough...

Brian Hayes says attending Golfgate event was ‘big error of judgement’

Brian Hayes, chief executive of Banking & Payments Federation Ireland (BPFI), considered resigning after he attended this year’s controversial...

Senzo Meyiwa: Police ‘know nothing’ of alleged murder weapon

The name Senzo Meyiwa was trending on Tuesday 20 October 2020 after it was suggested by a news website...

ICC prosecutor says Bashir and other suspects must face justice over Darfur

Ousted Sudanese President Omar al-Bashir and other suspects wanted by the International Criminal Court for alleged war crimes and...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you