News Amuua mkewe kisa wivu wa mapenzi

Amuua mkewe kisa wivu wa mapenzi

-

 

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Elia Shija(30) mkazi wa Kijiji cha Didia wilaya ya Shinyanga  anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma kisu shingoni mke wake na kisha na yeye kujijeruhi  kwa kujichoma kisu tumboni.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba,ambapo amesema limetokea saa 7 usiku wa kuamkia leo na amemtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni Mariam Julius(26)mkazi wa Kijiji cha Didia huku chanzo cha mauaji hayo ikisadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda Magiligimba amesema mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine ambaye hamjui kwa jina wala sura ndipo aliamua kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji.

Katika maelezo yake ya awali mtuhumiwa  aliwataja baadhi ya watu ambao alidai ndiyo walikuwa wakishirikiana kumtafutia wanaume mke wake ambao ni Lyidia Masesa(20) na Mariam Emmanuel (25) wote wakazi wa Kijiji cha Didia.

Mtuhumiwa amelazwa hospitali ya rufaa Mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya kutokana na majeraha makubwa baada ya kujichoma kisu tumboni kuliko pelekea utumbo wake kutoka nje.

Kamanda amesema taarifa za watu waliokuwa wanadaiwa kumsaidia mke wake kumtafutia wanaume mtuhumiwa alizikuta kwenye daftari lililokuwa chumbani mwao walimokuwa wanalala na marehemu mke wake.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Coronavirus Immunity May Only Last A Few Months after Infection: Study

- Science news - Research by Imperial College London estimated just 4.4% of adults had some form of...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you