News Balozi Seif aipongeza TASAF

Balozi Seif aipongeza TASAF

-

 

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Mfukowa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf} umeonesha muelekeo mzuri wa ufanisi mkubwa unaopatikana katika Utekelezaji wa Miradi ya Jamii tangu ulipoanzishwa ndani ya Awamu ya Tatu ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema Viongozi wa Wilaya, Halmashauri, Majimbo, Wadi pamoja na Shehia wana wajibu na jukumu la kuwasimamia vyema wananchi katika kuona miradi wanayoiibua katika Maeneo yao inaendelea kupata ufanisi kama inavyojidhihirisha hivi sasa katika mpango huo unaosaidia kustawisha Jamii.

Balozi Seif ameyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Shehia za Mkataleni na Mahonda, Walimu na Wanafunzi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Madarasa Matatu pamoja na Jengo la Utawala la Skuli ya Sekondari ya Mahonda  Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf}.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ililazimika kufanya mabadiliko katika ngazi ya Utawala kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa upande wa Zanzibar ili kuona Taasisi hiyo ya Kijamii inatekeleza wajibu wake katika misingi iliyopangiwa ya kuunga mkono jitihada za Jamii kwenye Miradi yao ya Maendeleo.

Balozi Seif amebainisha wazi kwamba wapo baadhi ya Watendaji wa TASAF katika kipindi kilichopita walikuwa wakizorotesha kazi kwa kufikiria zaidi maslahi yao binafsi bila ya kujali kwamba chombo hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuwakomboa Wananchi Kiuchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea faraja yake kutokana na Uzalendo mkubwa wa Watendaji na Viongozi wa Mfuko huo  na kuwapongeza jinsi walivyojizatiti katika kusimamia Utekelezaji wa Miradi iliyobuniwa na Jamii inayokwenda kwa kasi katika maeneo mbali mbali Nchini.

“ Nikiri kwa dhati Kwamba majengo haya niliyoyawekea jiwe la msingi hivi punde yanaendelea kujengwa katika ubora unaokubalika katika fani ya ujenzi na uharaka wake uliyofikia huwezi kuamini kama ni ya Mwezi Mmoja.” Amesema Balozi Seif.

Amesema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Sera yake ya Elimu imejizatiti katika kuona Wanafunzi wote wa Visiwa vya Unguja na Pemba wanapata taaluma katika mazingira bora na kiwango kinachokubalika Kitaifa na Kimataifa.

Akigusia Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika wiki chache zijazo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa amewatahadharisha wana CCM na Wananchi wote nchini kujiepusha kuingia katika mtego wa kuuza vitambulisho vyao vya kupigia kura.

Wakitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Tasaf Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania  Ladislaus Mwamanga na Mkurugenzi Uratibu wa Shughuli za Serikali Zanzibar anayesimamia TASAF Zanzibar Khalid Bakari Amran wamesema Zanzibar  itapatiwa Shilingi Bilioni 112 katika Kipindi cha Miaka minne ijayo.

Mradi wa ujenzi wa Jengo la madarasa matatu ya Skuli ya Sekondari Mahonda utagharimu zaidi ya Shilingi Milioni sabini ya saba wakati la Jengo la Utawala likitegemewa kugharimu jumla ya Shilingi Milioni 78 Nukta Nane.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

BDS victory as US university strikes down pro-Israel resolution 

Butler University is the latest American college to push back against the “vicious attempt to stifle Palestinian speech” by...

Father of 3 Gets Multiple Job Offers After Desperate Appeal

Joseph Owen Wanyonyi, a father of three children took to social media to make an appeal for help on...

Trump to Vote in Florida, Biden Heads to Pennsylvania

- Other Media news - Trump will vote in person in West Palm Beach, near his Mar-a-Lago estate,...

Sanctions against Iran amid COVID-19 Crisis ‘Cynical’: Russia’s Medvedev

- Politics news - "Some states that found themselves in a difficult situation, such as Venezuela, Iran, Cuba,...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you