News Benki ya Nmb Mkoani Mtwara yawapongeza wafanyabiashara kwa kusimama...

Benki ya Nmb Mkoani Mtwara yawapongeza wafanyabiashara kwa kusimama imara wakati wa mripuko wa Covid 19

-

 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Wafanyabiashara Mkoani Mtwara wamepongezwa juu ya kusimama imara katika kipindi kigumu kilichopita cha mripuko wa virus vya Corona (COVID-19).

Hayo yamesemwa na  Ndg Oscar Nyerenda amabye ni Mkuu wa kitengo cha hatari na majanga yanayoweza kuikabili Benk ya NMB wakati wa warsha(BUSINESS CLUB) waliyoifanya na wafanyabiashara Mkoani Mtwara katika ukumbi wa BOT Mkoani humo.

Nyerenda amesema licha ya Mripuko wa ugomjwa huo kutingisha Dunia lakini bado wafanyabisahara Mkoani Mtwara waliendelea na shughuli yao iyopepelea kutokutingishika kwa mitaji yao.

Aidha ameongeza kuwa kuna baadhi ya biashara zilipata mtikikisiko wakati wa mripuko wa COVID-19 ikiwemo biashara za hoteli pmoja na  utalii.

Lakini pia Nyerenda ameelezea kutokana na mripuko wa COVID-19 Benki ya NMB ilichukua hatua mbalimbali ili kuwanusuru wafanyabiashara juu janga hilo.

Moja a hatua zilizofanywa na NMB Benki kwa wafayanabiashara waliopo kwenye mikopo yao ni pamoja na kubadilisha utaratibu na mfumo wa maresho ambapo baadhi ya wateja walipunguziwa kiwango cha marejesho walichokuwa wadaiwa na Benki hiyo.

Nyerenda ameeleza kuwa Benki ya NMB katika kipindi cha mwaka 2020 mwezi juni imeweza kupata faida ya shilingi Bilioni tisini na tatu nukta sita na mafaniko hayo yamechagizwa na wafanyabaishara.

Kwa upande wa katibu wa wafanayabiashara Mkoa wa Mtwara Mwanaiza Mgeni ameipongeza Benki ya Nmb haswa kwa upande wa mikopo lakini kwa kupanua huduma zao ambapo kwa sasa uweza kuzipata kwa kutumia simu yako ya Mkononi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you

%d bloggers like this: