News China yaionya Canada kupokea waomba hifadhi kutoka Hong Kong

China yaionya Canada kupokea waomba hifadhi kutoka Hong Kong

-

Balozi wa China nchini Canada ameionya serikali ya Canada, dhidi ya kuwapa hifadhi wakaazi wa Hong Kong, walioikimbia sheria ya usalama inayokosolewa vikali, iliyowekwa na utawala wa Beijing kwenye jimbo lake hilo.

 Balozi Cong Pei-wu amesema kuwa waandamaji wanaounga mkono demokrasia huko Hong Kong, ni wahalifu wasiostahiki hifadhi. 

Ameonya kwamba kuwapa hifadhi watu kama hao, kutachukuliwa kama kuingilia mambo ya ndani ya China, jambo ambalo halikubaliki. Balozi Cong amesema endapo Canada inawajali wakaazi 300,000 wa Hong Kong wenye paspoti za Canada, na pia kampuni zake zilizoko Hong Kong, basi inapaswa kuunga mkono juhudi za China, kupambana na kiel alichokiita “uhalifu,” badala ya kuwapa hifadhi watu hao. 

Canada imekuwa ikiwapa hifadhi viongozi wa maandamano ya wanafunzi kutokea Hong Kong, na wale wanaoikimbia sheria mpya ya usalama, iliyoanza rasmi kutumika tarehe 30 Juni mwaka huu.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

AU Envoy Raila Wades Into Nigeria Police Murders

Former Prime Minister Raila Odinga has added his voice to the chaos and killings witnessed in Nigeria. In a statement,...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you