News DC Sabaya - Askari nao ni binadamu wanachukia

DC Sabaya – Askari nao ni binadamu wanachukia

-

 

Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amesema hakuna Askari aliyemzuia Mbowe kufanya kampeni na kwamba hata video inayosambaa mitandaoni ikimuonesha yeye na Askari wakibishana ni kwa sababu alivunja utaratibu kwa kutaka kufanya kampeni eneo ambalo hakutakiwa kinyume na kanuni za Tume.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 10, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, alipoulizwa alichukuliaje kitendo cha Askari kumzuia mgombea kufanya kampeni huku akidai mgombea huyo hawezi kumshinda mgombea wa chama fulani, ambapo amesema kuwa Askari huyo alifika pale kwa lengo la kuwaweka sawa kwani eneo hilo kulikuwa na mgombea mwingine.

“OCD alifika pale kuhakikisha makundi mawili hayahitilifiani na Mbowe alifanya makusudi na aliambiwa aondoke ndiyo mabishano yakatokea, Jeshi la polisi ni chombo cha dola na wanaolitumikia ni binadamu nao wanafika mahali wanakasirika, kwamba kila mahali ni kuwanyoshea kidole kama alivyozoea ni bora angeendelea kunitukana mimi lakini siyo yule mtu mzima watu wasione matukio ya mwisho ya mtu aliyedhihakiwa halafu wang’ang’anie huyu mwingine”, amesema DC Sabaya

“Aliyevunja taratibu ni huyu mgombea ubunge, naamini Tume nayo itachukua hatua hamuwezi kuweka sheria wenyewe na mnazivunja, halafu mnatafuta huruma nyepesi kwa sababu mmeshindwa kuomba kura, unageuza agenda ya kuomba kura ili ujipatie huruma hiyo haikubaliki kabisa”, ameongeza DC Sabaya.

Oktoba 7 mwaka huu ilionekana video mitandaoni ikimuonesha Askari Polisi wilayani Hai, akibishana na mgombea ubunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe kuhusu ufanyaji wa kampeni huku Askari huyo akidai kuwa Mbowe hawezi kumshinda mgombea wa chama kingine ambaye hakumtaja jina.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Russia and Iran obtain voter information ahead of US election, officials say

Russia and Iran have obtained US voting registration information and are aiming to interfere in the presidential election, the...

Long-awaited Ghostbusters sequel delayed

The long-awaited Ghostbusters sequel has been delayed by three months, studio Sony said. Ghostbusters: Afterlife will now arrive on June...

Short-form streaming service Quibi to close after six months

Short-form streaming service Quibi is closing down just over six months since launching, the company has announced. The service had...

Rudy Giuliani responds to Borat video

Donald Trump ally Rudy Giuliani has described a video clip from the upcoming Borat film appearing to show him...

Martin Bashir ‘seriously unwell’ with Covid-19 related complications

Veteran journalist Martin Bashir is “seriously unwell” with coronavirus-related complications, the BBC has said. The 57-year-old, best known for his...

Manchester City come from behind to beat Porto

Manchester City 3 - 1 FC Porto Manchester City made a winning start to their latest assault on the Champions League as they came...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you