News Ditopile anyakua wengine kutoka Chadema, ni wanachama Saba, waomba...

Ditopile anyakua wengine kutoka Chadema, ni wanachama Saba, waomba kuhamia CCM

-

 UZINDUZI wa Kampeni za Udiwani Kata ya Chang’ombe jijini Dodoma CCM zilizozinduliwa na Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile zimefanikiwa kuondoka na wanachama saba wa Chadema ambao wamekihama chama hicho na kuhamia CCM.

Wanachama hao wamerejesha kadi zao za Chadema huku wakimueleza Mariam Ditopile kuwa wameamua kurudi CCM kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia watanzania wanyonge kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Uchumi na Miundombinu huku wakisema Dodoma ya leo chini ya Dk Magufuli imepiga hatua kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Ditopile amewaomba wananchi wa kata ya Chang’ombe kumchagua Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Diwani wa kata hiyo, Bakari Fundikira ili wamalizie miaka mitano mingine ya kuwatumikia wananchi wa Chang’ombe.

Ditopile amesema miaka mitano iliyopita serikali ya CCM imeibadilisha kata ya Chang’ombe kutoka kuwa eneo la kawaida na kuwa eneo ambalo limekua fursa ya kiuchumi na hivyo kuwakwamua wananchi wake na umaskini.

” Hakuna asiyejua Chang’ombe mlikua na shida kubwa ya barabara lakini miaka mitano ya Magufuli, Mavunde na Fundikira leo mna barabara za lami tena zilizojengewa mitaro ya kisas a ya kupitisha maji lakini zaidi ya km tatu ya barabara ya Chang’ombe inawaka taa za barabarani.

Ni Mbunge Mavunde ambaye amewafuta akina Mama na Vijana machozi ambapo kwa kushirikiana na Diwani Fundikira wamewezesha ujenzi wa Soko la Mavunde lililopo kwenye kata hii ambalo sasa limekua na manufaa kwa wajasiriamali,” Amesema Ditopile.

Amewaomba watanzania na hawa wananchi hao wa Chang’ombe kuepuka hila na Sera za uongo zinazoletwa na vyama vya upinzani huku akisema vyama hivyo vimeshindwa kujenga hata ofisi zao wenyewe hivyo hawafai kupewa Nchi waongoze.

” Siku hizi wananiita Mbatizaji maana kila napoenda nawarudisha, nimefanya hivyo Udom kule, Bahi, Chemba, wanachama wa Chadema waliorudi CCM leo wamerudi kwa sababu ya kazi kubwa inayofanywa na Dk Magufuli katika kuwatumikia watanzania, niwaombe watu wa Chang’ombe Oktoba 28 mjitokeze kwa wingi kumpigia kura Magufuli, Mavunde na Fundikira.

” Ni Rais Magufuli na wasaidizi wake Mbunge Mavunde na Diwani Fundikira wamemaliza changamoto ya barabara ya Chang’ombe leo lami ipo ya kutosha huku km 3 zikiwa zinawaka taa za barabara, Mbunge Mavunde kasaidia ujenzi wa soko la kisasa la Chang’ombe lililopewa jina la Mavunde Makert, tuachane na upinzani hawana sera ndio maana Lissu amefanya mkutano wake leo hapa lakini idadi ya watu waliojitokeza unazidiwa na wa mgombea udiwani wa CCM, ” Ditopile.

Kwa upande wake Mgombea wa Udiwani wa  kata hiyo, Bakari Fundikira amemshukuru Ditopile kwa kwenda kuzindua kampeni zake ambapo amemuahidi kuwa CCM itaongoza kwa kura za kishindo Chang’ombe kuanzia kura za Urais, Ubunge na Udiwani.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Vicky McClure, Martin Compston and Adrian Dunbar film Line Of Duty in Belfast

Vicky McClure, Martin Compston and Adrian Dunbar were back on the beat as Line Of Duty continued filming in...

Sagini aahidi kumalisha mradi wa maji kutoka ziwa victoria

Mbunge Mteule wa Jimbo la Butiama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jumanne Sagini amesema akiapishwa atahakikisha anakamilisha mradi wa...

Russian airstrike injures 5 civilians in Syria’s Idlib

Five civilians were injured in a Russian airstrike in Syria’s northwestern Idlib province, according to the White Helmets civil...

Football fan dies five years after he was attacked by opposition thugs

A football fan who was attacked by opposition thugs and suffered devastating injuries on his way back from an...

Mkuu wa NATO afuta uwezekano wa kuondoka mapema Afghanistan

 Wakati machafuko yanayooengezeka yakitishia kuyakwamisha mazungumzo ya amani nchini Afghanistan, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens...

Nicola Adams and Katya Jones’ first same-sex routine on Strictly revealed

Nicola Adams and Katya Jones will quickstep to Get Happy by Ella Fitzgerald in their first scored performance on...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you