News Iran yasema marufuku ya silaha ya UN dhidi yake...

Iran yasema marufuku ya silaha ya UN dhidi yake imefikia kikomo

-

 

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema kuwa marufuku ya muda mrefu ya uuzaji silaha kutoka na kuingia nchini humo imefikia muda wake wa mwisho mapema leo kuambatana na mkataba wa kihistoria wa nyuklia wa mwaka 2015. 

Katika taarifa, wizara hiyo imesema kuwa kuanzia leo, vikwazo vyote vya kusafirisha silaha, shughuli kuzihusu na huduma za kifedha kuingia na kutoka nchini humo vimeondolewa mara moja. 

Muda wa marufuku hiyo ya uuzaji wa silaha ulikuwa uanze kufikia kikomo polepole kutokea Jumapili Oktoba 18 chini ya matakwa ya maazimio ya Umoja wa Mataifa yaliofanikisha kubuniwa kwa mkataba huo wa nyuklia kati ya Jamuhuri hiyo ya kiislamu na mataifa yenye ushawishi duniani. 

Mnamo mwezi Septemba, Urusi ilisema kuwa iko tayari kuimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na Iran huku China pia ikizungumzia kuwa tayari kuiuzia Iran silaha baada ya Oktoba 18. 

Marekani imesisitiza kwamba itatafuta kuizuia Iran kununua silaha za China na mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Blind Granny Dies Days Before Receiving New House

A 72-year-old woman who passed away days before she could move into a house that was built by well-wishers...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you