News Kampeni ya Namthamini kufanya matembezi ya hisani

Kampeni ya Namthamini kufanya matembezi ya hisani

-

 

Kampuni mbalimbali pamoja na watu binafsi wamejitokeza kuchangia vitu mbalimbali kwa ajili ya elimu ya mtoto wa kike Kisarawe kupitia kampeni ya Namthamini ya EATV Limited kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.

Miongoni mwa kampuni zilizojitokeza kuunga mkono kampeni hiyo ni kampuni ya magazeti ya The Guardian Limited pamoja na ITV/Radio One zilizopo Mikocheni eneo la viwanda jijini Dar es Salaam na kuchangia msaada wa taulo za kike kama sehemu ya mchango wao katika kampeni hiyo.

 ”Wadau mbalimbali wajitokeze ili kusaidia kutimiza ndoto za watoto wa kike waliopo mashuleni ambao muda wao wa masomo hupotea kutokana na kukosa mahitaji muhimu ikiwemo taulo za kike, waanapoingia kwenye siku zao za hedhi kila mwezi”Amesema Bwana Samuel Mtui, Meneja Rasilimali Fedha wa The Guardian LTD.

Sambamba na hilo,wadau wengine waliojitokeza kuchangia kampeni hii wakiwemo Flora Njelekela kutoka taasisi ya ANUFLO, Agatha Tuheri Laizer kutoka taasisi ya Seasoning Palet na wengineo.

Katika kuelekea Siku ya Mtoto wa Kike Duniani kesho, East Africa Television (EATV) Limited, kupitia kampeni yake ya Namthamini itafanya Matembezi ya Hisani Kisarawe kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo yenye lengo la kuchangia Elimu ya Mtoto wa Kike Wilayani humo.

Kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ni “Tumwezeshe Mtoto wa Kike; Kujenga Taifa Lenye Usawa”

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Move against INM inspectors is attempt to damage ex-CEO Robert Pitt, court told

Former INM Chairman Leslie Buckley’s bid to have two inspectors withdrawn from investigating matters at INM is a “deliberate”...

Mark Hamill remembers Carrie Fisher on what would have been her 64th birthday

Mark Hamill has remembered Carrie Fisher on what would have been her 64th birthday. The Star Wars actor shared a...

German police detain Syrian suspected of killing tourist

German police have arrested a 20-year-old Syrian suspected of attacking two tourists in the eastern city of Dresden at...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you