News Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi azindua awamu...

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi azindua awamu ya tatu ya uogeshaji Mifugo

-

Na Ezekiel Mtonyole, Bahi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,  amezindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo, huku akiwataka wafugaji nchini kuhakikisha wanaogesha mifugo ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma,  Prof.Elisante amesema lengo la serikali ni kuongeza tija ya ufugaji kwa kuwa na mifugo yenye afya itakayozalisha mazao zaidi yenye ubora wa kitaifa na kimataifa.

“Lengo la kuogesha mifugo ni kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe hususani Ndigana kali ambayo imekuwa ni changamoto katika kuendeleza tasnia ya mifugo nchini,”amesema.

Amebainisha kuwa mara nyingi magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri mifugo na kusababisha hasara kubwa kwa mfugaji kutokunufaika na shughuli zao.

“Magonjwa yanayoenezwa na kupe yasipodhibitiwa ipasavyo huchangia asilimia 72 ya vifo vyote vya ng’ombe nchini, kati ya magonjwa hayo, ugonjwa wa Ndigana kali huchangia vifo kwa kiwango kikubwa cha asilimia 44,”amesema.

Katibu Mkuu huyo amesema hasara inayotokana na magonjwa hayo inakadiriwa kuwa takribani Sh.Bilioni 145, na kusababisha kupungua uzalishaji maziwa, nyama kutokana na kukonda, kushuka kwa thamani ya ngozi, kupoteza wanyama kazi na udumavu wa ndama.

Amefafanua kuwa uogeshaji wa mifugo kwa kutumia josho ni mzuri na hasa kwa wafugaji wenye mifugo mingi  na unadhibiti magonjwa hayo.

Amesema mwaka 2018 Wizara hiyo ilitengeneza mkakati wa kudhibiti magonjwa hayo kwa kuanzisha kampeni hiyo ambapo kwa awamu ya kwanza na pili serikali ilinunua lita 21,373.06 zenye thamani ya Sh.Milioni 740.7 kwa ajili ya kuogesha mifugo.

“Katika awamu zote mbili kumekuwa na jumla ya michovyo Milioni 245.37 ya mifugo yote ikiwemo ng’ombe Milioni 176.32, Mbuzi Milioni 58.02, kondoa Milioni 20.03 na punda 2,685,”amesema.

Kuhusu kampeni huyo awamu ya tatu, amesema serikali imenunua dawa ya kuogesha mifugo aina ya Paranex, Paratop, Amitraz kiasi cha lita 15,579 zenye thamani ya Sh.Milioni 592.82 ambazo zitatosheleza majosho 1,983 katika halmashauri 162 na michovyo inayotarajiwa ni Milioni 405 ya mifugo yote itakayoogeshwa.

Ameagiza Halmashauri kusimamia kanuni ya uogeshaji ili wafugaji waifuate na kushirikiana nao na wadau kujenga na kukarabati majosho yake na miundombinu mingine ya mifugo.

Awali, akitoa taarifa ya uogeshaji mifugo wilayani Bahi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Dk.Fatuma Mganga, amesema mifugo inachangia zaidi ya asilimia 55 ya mapato ndani ya Halmashauri hiyo kwa mwaka.

Amesema kuna minada 15 ambayo hufanyika biashara ya kuuza wastani wa ng’ombe 3,882, mbuzi 4,602 na kondoo 89 kwa mwezi.

Hata hivyo, amesema halmashuari imekwisha andika andiko la mradi wa kiwanda cha uchakataji ngozi lenye thamani ya Sh.Bilioni 3.3 tayari andiko hilo lipo Wizara ya Fedha kwa ajili ya mapitio ya mwisho kabla fedha kutolewa.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Dk.Hezron Nonga, amesema  mwaka 2019, majosho zaidi ya 511 yalikarabatiwa nchi nzima kwenye Halmashauri huku 78 mapya yalijengwa.

“Vifo vya ng’ombe hususan ndama vilipungua kwa asilimia 30 kwasababu ya uogeshaji, tukiogesha vifo vya ng’ombe zetu tunatokomeza,”amesema.

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Russia and Iran obtain voter information ahead of US election, officials say

Russia and Iran have obtained US voting registration information and are aiming to interfere in the presidential election, the...

Long-awaited Ghostbusters sequel delayed

The long-awaited Ghostbusters sequel has been delayed by three months, studio Sony said. Ghostbusters: Afterlife will now arrive on June...

Short-form streaming service Quibi to close after six months

Short-form streaming service Quibi is closing down just over six months since launching, the company has announced. The service had...

Rudy Giuliani responds to Borat video

Donald Trump ally Rudy Giuliani has described a video clip from the upcoming Borat film appearing to show him...

Martin Bashir ‘seriously unwell’ with Covid-19 related complications

Veteran journalist Martin Bashir is “seriously unwell” with coronavirus-related complications, the BBC has said. The 57-year-old, best known for his...

Manchester City come from behind to beat Porto

Manchester City 3 - 1 FC Porto Manchester City made a winning start to their latest assault on the Champions League as they came...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you