News Kauli alizozizungumza Dk. Hussein Mwinyi kwenye Mkutano wa Kampeni...

Kauli alizozizungumza Dk. Hussein Mwinyi kwenye Mkutano wa Kampeni Chwaka

-

Thabit madai, Zanzibar

Kauli alizozizungumza Dk. Hussein Ali Mwinyi kwenye Mkutano wa Kampeni Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.

“Baadhi ya matatizo yanasababishwa na baadhi ya viongozi kukiuka utaratibu. Ninawahakikishia kuwa kila kiongozi atawajibika kikamilifu na ambaye hatawajibika litakuwa ni jukumu letu kumchukulia hatua kwa sababu kila kiongozi ni lazima awajibike.”

“Kazi iliyofanyika kwenye miundombinu kila mtu anaona na sasa nchi nzima imefunguka kwa barabara za lami.”

“Kuhusu suala la ajira, tunataka kujenga uchumi mpya na uchumi wa kisasa ambao utatoa ajira nyingi sana. Kwenye sekta ya uvuvi ilani yetu imepanga kutoa ajira 300,000 na mimi sina shaka katika hilo.”

“Kuna maeneo tutakayoyafanyia kazi kuanzia wajasiriamali, wavuvi wadogo na waanika dagaa. Tunataka kuboresha mfuko wa kusaidia wajasiriamali wadogo. Ninawahakikishia wajasiriamali wadogo kuwa mambo mazuri yanakuja.”

“Ndugu zangu nataka nirudie; yajayo yanafurahisha, yajayo ni neema tupu kwa Wazanzibar.”

“Tunaposema Zanzibar mpya tunamaanisha uchumi mpya unaokuja ni uchumi wa kisasa, uchumi wa utalii na uvuvi mkubwa ambapo ndani yake kuna uvuvi wa bahari kuu.”

“Natambua zimejengwa barabara kuu nyingi, kazi yetu itakuwa kumalizia barabara kuu zilizobaki na kuanza kuingia kujenga za ndani.”
“Tunataka tuwe na maeneo maalumu ya utalii na uvuvi kwa maana hiyo tutawawezesha wavuvi wetu waende mbali zaidi kwenye maji makubwa ili wasiingiliane na kazi za utalii kwenye fukwe au maeneo tengefu ili kuhakikisha rasilimali za nchi haziharibiki”

“Kutokana na ukosefu wa soko mnalazimika kuuza mazao yenu mjini, hili lazima tuliangalie kwa kuhakikisha wilaya hii ya kati inapata soko lake.” Dkt. Mwinyi kutoka Chwaka.

“Ili haya yote tuliyoyazungumza yaweze kutekelezeka ni lazima tushike dola. Kwa heshima na taadhima ninawaomba mtupigie kura pamoja na familia zenu zote zilizopo nyumbani.”

“Hapa  Zanzibar idadi yetu ya watu haizidi millioni 2. Soko kubwa liko bara la watu millioni 60, unachozalisha chochote unaweza kupeleka bara ukauza lakini vile ambavyo havipatikani huku tutavileta kutoka bara na hii ndiyo faida ya Muungano.”
Dkt. Mwinyi Zanzibar

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

AU Envoy Raila Wades Into Nigeria Police Murders

Former Prime Minister Raila Odinga has added his voice to the chaos and killings witnessed in Nigeria. In a statement,...

Jewish Settlers Storm Al-Aqsa Mosque Compound under Israeli Police Protection

- World news -  “Under the protection of Israeli police, over 100 settlers stormed the compound through Al-Mugharbah...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you