News Kauli ya LeBron kuhusu mashabiki wa Lakers

Kauli ya LeBron kuhusu mashabiki wa Lakers

-

Nyota wa mchezo wa mpira wa kikapu, LeBron James ameweka wazi somo ambalo amejifunza kutoka kwa mashabiki wa Los Angeles Lakers, kuwa hawajali wasifu wa mchezaji hadi atakapowaletea ubingwa wa NBA.

LeBron ambaye alitwaa ubingwa wa NBA mara tatu akiwa na timu tofauti, alisema kutwaa ubingwa kwa Lakers ndio njia pekee ambayo anaweza kupata kiwango kipya cha heshima kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo huko Los Angeles.

”Nilichojifunza kwa mashabiki wa Los Angels Lakers ni kwamba hawatojali wasifu wako kwa ulichokifanya awali, watakupa heshima iwapo utawapelekea ubingwa”, amesema LeBron James.

Los Angeles Lakers inaongoza fainali kwa 3-1 dhidi ya Miami Heat na huenda ikatwaa taji la ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, iwapo itashinda mchezo wa tano alfajiri ya Oktoba 10, 2020.

Ikumbukwe LeBron alikuwepo kwenye kikosi cha Cleveland Cavaliers kilichotoka nyuma kwenye kipigo cha 3-1 na kuibuka mabingwa mwaka 2016 dhidi ya Golden State Warriors.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Libya’s state council urges al-Sarraj to remain

The High Council of State urged the head of the Presidential Council, Fayez al-Sarraj, to stay on Thursday until...

Mavunde kinara Ubunge Dodoma Mjini

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini, Wakili Msekeni Mkufya amemtangaza Anthony Mavunde wa CCM kuwa mshindi wa kiti...

Askofu Josephat Gwajima aibuka kidedea kiti cha Ubunge jimbo la Kawe

 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kawe amemtangaza Askofu Josephat Gwajima wa CCM kuwa mshindi wa Ubunge katika Jimbo hilo...

Kilave Dorothy George aibuka mshindi kiti cha Ubunge Jimbo la Temeke

 Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Temeke amemtangaza mgombea Ubunge jimbo hilo kupitia CCM Kilave Dorothy George kuwa mshindi kwa...

Mwana FA ashinda kiti cha Ubunge jimbo la Muheza

 Mwana FA wa CCM, amemshinda Yosepher Komba wa CHADEMA ubunge jimbo la Muheza kwa kura 47,578.

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you

%d bloggers like this: