News Kiwanda kilichosimama kwa muda mrefu kuanza kazi

Kiwanda kilichosimama kwa muda mrefu kuanza kazi

-

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa, amewataka wakulima wa chai wilayani Lushoto wajiandae na kilimo hicho kwa kuwa kiwanda cha Mponde kilichopo katika jimbo la Bumbuli, kinatarajiwa kuanza uzalishaji hivi karibuni baada ya kusimama kwa muda mrefu.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto, mkoani Tanga katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Soni wakati akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli na wagombea udiwani  baada ya mgombea ubunge wa jimbo hilo January Makamba kupita bila ya kupingwa.

“Najua msimu huu mmehangaika sana, lazima kiwanda chetu kianze kazi na hatua zote za msingi zimeshakamilika, msimamizi mkuu ni Msajili wa Hazina na mwekezaji ni mifuko ya hifadhi ya jamiii ya PSSSF na WCF, ambao walishakuja kufanya ukaguzi ila kuna mitambo inahitaji vipuri na tumeagiza vichongwe ili kazi ianze chai isindikwe”, amesema Kassim Majaliwa.

Kiwanda cha chai cha Mponde ni miongoni mwa viwanda vya kusindika majani mabichi ya chai katika Halmashauri ya Bumbuli na hutegemewa na wakulima wadogo wa chai wapatao 5,000 kama soko la majani mabichi ya chai kutoka katika mashamba yao, ambapo uzalishaji ulisimama kufuatia mgogoro uliojitokeza mwaka 2013.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

BDS victory as US university strikes down pro-Israel resolution 

Butler University is the latest American college to push back against the “vicious attempt to stifle Palestinian speech” by...

Father of 3 Gets Multiple Job Offers After Desperate Appeal

Joseph Owen Wanyonyi, a father of three children took to social media to make an appeal for help on...

Trump to Vote in Florida, Biden Heads to Pennsylvania

- Other Media news - Trump will vote in person in West Palm Beach, near his Mar-a-Lago estate,...

Sanctions against Iran amid COVID-19 Crisis ‘Cynical’: Russia’s Medvedev

- Politics news - "Some states that found themselves in a difficult situation, such as Venezuela, Iran, Cuba,...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you