News Lissu amkumbuka Mzee Sitta kwa hili

Lissu amkumbuka Mzee Sitta kwa hili

-

 

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kuwa marehemu Samuel Sitta ndiye aliyewahi kuwa Spika wa Bunge bora zaidi kwa kuwa aliruhusu wabunge kuongea.

Lissu ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 16, 2020, wakati akizungumza na wanachi wa Urambo mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, katika maeneo mbalimbali nchini.

“Nyie mnafahamu mzee Sitta alikuwa ni mbunge hapa kwa miaka 30, Sitta alikuwa Spika wa Bunge, katika historia yetu ya kibunge hatujawahi kuwa na Spika wa aina ya kama marehemu Mzee Sitta, na sifa yake ni moja tu aliruhusu wabunge kusema kwa sababu ni mahali pa kusema”, amesema Lissu.

Katika hatua nyingine Lissu amesema kuwa, “Nataka tuwe watu huru, rais tunamchagua wenyewe akikosea tuwe na haki ya kumsema, mbunge akikosea tuwe na haki ya kumsema, Mkuu wa wilaya na Mkuu wa mkoa wakikosea tuwe na haki ya kuwakosoa kwa sababu hawa tunaambiwa ni watumishi wetu”.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Sudanese Protesters Set Israeli Flag on Fire over Normalization (+Video)

- World news - They rallied in the capital Khartoum Friday evening, calling on Sudan’s Sovereign Council chief...

Europe Becomes Second Region to Cross 250,000 COVID-19 Deaths

- Other Media news - Europe reported 200,000 daily infections for the first time on Thursday, as many...

Bahrain: Anti-normalisation protests despite security restrictions 

Anti-normalisation protests erupted in the streets of the Bahraini capital of Manama after Friday prayer yesterday. Protesters held up banners...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you