News Maandamano ya kupinga mauaji ya kijana mweusi Marekani

Maandamano ya kupinga mauaji ya kijana mweusi Marekani

-

Ilani ya marufuku ya kutoka nje imetangazwa katika mji wa Philadelphia nchini Marekani ili kudhibiti hali ya usalama kutokana na maandamano yaliyoanzishwa kufuatia mauaji ya kijana mweusi Walter Wallace.

Wallace amaye ni raia mwenye asili ya Kiafrika, alifyatuliwa risasi na maafisa 2 wa polisi kwa alipotaka kuwasogelea akiwa na kisu mkononi.

Maandamano yaliendelea kwa siku 3 katika ambapo mamlaka ilichukuwa hatua ya kutangaza marufuku ya kutoka nje kuanzia Alhamisi saa 21:00 hadi 06:00 kote mjini.

Viongozi wa idara ya usalama wamearifu kuwa hadi kufikia sasa maafisa 53 wa polisi wamejeruhiwa na magari 17 ya polisi kuharibiwa huku watu 172 wakitiwa mbaroni kwenye maandamano hayo yaliyoanza tangu siku ya Jumatatu nyakati za usiku.  

Siku ya Jumatatu, maafisa wa polisi walipokea taarifa ya tukio na kumuua Walter Wallace mwenye umri wa miaka 27 kwa kumfyatulia risasi baada ya kumsogelea afisa mmoja akiwa amebeba kisu mkononi.

Walter Wallace Sr ambaye ni babake Wallace, alitoa maelezo baada ya tukio hilo na kubainisha kuwa mwanawe alikuwa na matatizo ya kiakili yaliyotokana na matumizi ya madawa.

Maelezo zaidi yanaarifu kuwa Wallace ambaye aliuawa kwa risasi 10 zilizoingia mwilini mwake, alikuwa ni baba wa mapacha wawili wa kiume. Babake alihoji maafisa wa polisi kwa kuwauliza, “Kwa nini hawakutumia bastola za shoti?”

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Americans travel home for Thanksgiving despite coronavirus surge

Millions of Americans took to the skies and the roads ahead of Thanksgiving at the risk of pouring petrol...

Last orders for Dublin’s Rí-Rá nightclub and The Globe bar

It’s ‘last orders’ for well known Dublin night venues, Rí-Rá nightclub and The Globe bar. Dublin City Council has approved...

Cinema Verite to hold classes attended by cinematic figures

Several master classes attended by experienced Iranian and foreign coaches will also be held in online format which provides...

Brexit problems likely to fall to courts to resolve, says NI judiciary chief

Problems from Brexit will probably fall to courts to resolve, the head of Northern Ireland’s judiciary has said. Lord Chief...

Azam FC yamfuta kazi kocha wake Aristica Cioaba

Kocha Aristica Cioaba amefutwa jumlajumla kazi ndani ya Azam FC msimu wa 2020/21 kutokana na matokeo mabaya aliyopata hivi...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you