News Makombora yashambulia miji ya Azerbaijan, 7 wauawa

Makombora yashambulia miji ya Azerbaijan, 7 wauawa

-

Watu wapatao saba wameuawa, baada ya kombora kuangukia kwenye nyumba kadhaa, katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Azerbaijan, Ganja, hivi leo. 

Mashambulizi hayo, ambayo yamefanyika masaa machache, baada ya kushambuliwa mji mkuu wa jimbo la Nagorno-Karabakh, Stepanakert, yanaashiria kuendelea kwa mapigano, kwenye mzozo wa wiki tatu sasa, baina ya Armenia na Azerbaijan.

 Waandishi wa shirika la habari la AFP mjini Ganja, wameripoti kushuhudia majumba yakigeuzwa vifusi, huku watu wakikimbia huku na kule. 

Wafanyakazi wa huduma za uokozi, wanaendelea kusaka manusura. Msaidizi maalum wa Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan, amesema zaidi ya nyumba 20 zimeharibiwa na mashambulizi hayo, ya alfajiri ya leo. 

Jumapili iliyopita, watu wengine 10 waliuawa kwenye mji huo huo, kutokana na makombora. Uturuki na Urusi, ambazo zinaunga mkono pande tafauti za mzozo huo, zimetowa wito wa kusitishwa mapigano.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you