News Makubaliano ya amani kati ya Saudia na Israeli yako...

Makubaliano ya amani kati ya Saudia na Israeli yako njiani kufikiwa?

-

 

Watafanikiwa au la? ni swali lililo kwenye vichwa vya watu wengi katika eneo la Mashariki ya kati hivi sasa.

Je! Watawala wa Saudi Arabia, wakosoaji wa kihistoria wa Israeli kuhusu matendo yake dhidi ya Wapalestina, hatimaye wanakaribia kurekebisha mahusiano na nchi hiyo ?

Kumekuwa maoni mengi katika mitandao ya kijamii kutokana na mahojiano kupitia televisheni ya Al-Arabiya na mkuu wa zamani wa ujasusi wa Saudi na balozi wa muda mrefu huko Washington, Mwanamfalme Bandar Bin Sultan al-Saud, ambaye aliwakemea viongozi wa Palestina kwa kukosoa harakati za hivi karibuni za amani ya Israeli na Mataifa ya Ghuba ya Kiarabu.

“Hili si jambo tunalolitarajia kutoka kwa maafisa hao ambao wanatafuta kuungwa mkono na dunia kwa kitendo chao,” alisema Bandar katika mahojiano hayo ya sehemu tatu.

Viongozi wa Palestina hapo awali walielezea mchakato wa kumaliza uhasama wa nchi ya falme za kiarabu na Bahrain na Israel ni ”usaliti’.

Mwanamfalme Bandar, ambaye alikuwa balozi wa Saudia huko Washington kwa miaka 22 na alikuwa karibu sana na Rais wa zamani wa Marekani George W Bush kiasi kwamba mara nyingi alikuwa akipewa jina la Bandar Bin Bush, alizungumza juu ya “kutofaulu kihistoria” kwa uongozi wa Palestina. na kuwa imekuwa ikidharau juhudi za Saudi kuinga mkono. Aliwaambia watazamaji wa mahojiano hayo ya televisheni.

imechukua msaada wa Saudia kwa urahisi, aliwaambia wasikilizaji wake.

Pia alilaumu uongozi wa Israeli na uongozi wa Palestina kwa kushindwa kufikia makubaliano ya amani kwa miaka mingi.

Ni kwa namna gani hatua hiyo inaweza kupigwa kama mamlaka Palestina inayodhibiti Ukingo wa Magharibi, na Hamas inayodhibiti eneo la Gaza zenyewe zinashindwa hata kukubaliana wenyewe kwa wenyewe?.

Maneno hayo, alisema afisa wa Saudi aliye yuko karibu na familia inayotawala, vingievyo isingepeperushwa kwenye runinga inayomilikiwa na Saudia bila idhini ya Mfalme Salman na Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman.

Kwa kuchagua Mwanamfalme Bandar, mwanadiplomasia nguli kuyasema maneno hayo, ni ishara ya wazi kuwa utawala wa Saudia unaweza kuwa unawaandaa watu wake kuingia kwenye makubaliano ya na Israel.

Kwa miaka mingi, hasa katika maeneo ya vijiji vya Saudia, Raia wa nchi hiyo walishajenga imani kuona si tu Israel kama adui, bali wayahudi wote.

Kwasababu ya uwepo wa Intaneti na Televisheni za satelaiti nadharia hizo kwa sasa ziko kwa uchache mno; Rais wa Saudia sasa wanatumia muda mrefu mtandaoni na wanaweza kupata taarifa kwa namna njema kuhusu mahusiano ya dunia kuliko watu wa Magharibi.

Walakini kutokana na chuki dhidi ya wageni ambazo zipo katika sehemu fulani za Saudia itachukua muda kubadili dhana hii na ndio sababu Saudi Arabia haijakimbilia kufuata majirani zake wa Ghuba katika mpango huu wa makubaliano ya kihistoria.

Mpango wa amai wa Saudia

Saudi Arabia ina historia linapokuja suala la amani na Israeli.

Mnamo mwezi Machi mwaka 2002 nilikuwa kwenye mkutano wa nchi za Kiarabu huko Beirut, ambapo mtu mdogo, mwenye lugha ya Kiingereza safi alikuwa akizungumza , akielezea kitu kinachoitwa Mpango wa amani wa Mfalme Abdullah.

Mtu huyo alikuwa Adel Jubair, wakati huo alikuwa mshauri wa masuala ya kigeni katika Mahakama ya Mwanamfalme, ambaye sasa ni waziri wa mambo ya nje wa Saudia.

Mpango wa amani ulitawala mkutano huo mwaka huo na uliungwa mkono kwa pamoja na Jumuiya ya Kiarabu.

Uliiwezesha Israeli kupatana na ulimwengu wote wa Kiarabu kwa makubaliano ya kujiondoa katika maeneo yote yaliyokaliwa, ikiwemo Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza, Milima ya Golan na Lebanoni, na pia kuwapa Wapalestina Yerusalemu Mashariki kama mji mkuu wao na kufikia ” suluhisho tu “kwa wakimbizi wa Kipalestina ambao, katika vita vya Kiarabu na Israeli vya 1948-49, walikuwa wamefukuzwa au kutoka katika nyumba zao katika ile iliyokuwa Israeli.

Mpango huo ulipata uungwaji mkono mkono mkubwa kutoka kwenye jumuia ya kimataifa na kumfanya Waziri Mkuu Ariel Sharon kuzungumziwa, Hapa hatimaye ilionekana nafasi ya kumaliza kabisa mgogoro wa kihistoria wa nchi za kiarabu na Israeli.

Lakini kabla tu ya mpango huo kufikiwa, Hamas ilipiga bomu hoteli ya Israeli huko Netanya, na kuua watu 30 na kujeruhi zaidi ya 100. Mazungumzo yote ya amani yalikwama.

Mashariki ya Kati imesonga mbele kwa njia nyingi, ingawa Wapalestina bado hawajapata uhuru wa kujitawala na makazi ya Israeli yanayotazamwa kuwa haramu chini ya sheria za kimataifa yanaendelea kuingilia ardhi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi.

UAE, Bahrain, Jordan na Misri wamefikia makubaliano ya amani na Israel na sasa wana mahusiano kamili ya kidiplomasia.

Ndani ya siku chache baada ya Bahrain kutia saini Mkataba wa Abraham katika Ikulu ya White House, wakuu wa upelelezi wa Israeli walikuwa wakitembelea Manama, wakizungumza ushirikiano wa kiintelijensia kuhusu hasimu wao, Iran.

Kwa hivyo maafisa wa Israeli wanahisije kuhusu mapatano haya muhimu na Saudi Arabia?

Kwa hakika wametazama mahojiano na Mwanamfalme Bandar, lakini mpaka sasa wamekataa kutoa maoni yao moja kwa moja.

Badala yake, msemaji wa ubalozi wa Israeli huko London alisema: “Tunatumaini kwamba nchi nyingi zaidi zitatambua ukweli mpya katika Mashariki ya Kati kwa kuungana nasi kwenye kuelekea upatanisho.”

Saudi Arabia imekuwa ikipiga hatua taratibu na kwa umakini mkubwa katika masuala ya mabadiliko ya sera, wakifanyia majaribio kila hatua kabla ya kujikita kwenye mabadiliko husika.

Lakini kuwasili kwa eneo mwana mfalme Mohammed Bin Salman kumebadilisha yote hayo.

Wanawake sasa wanaendesha magari, kuna burudani za hadhara na sasa nchi inafungua milango kwa shughuli za kitalii.

Kwa hivyo mpango wa amani wa Saudia na Israeli, ingawa sio lazima uwe karibu, sasa kuna uwezekano wa kufikiwa.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Governor Nanok Cries Foul Over Ksh.8.2Billion Museum Project

Turkana Governor Josphat Nanok on Thursday, October 22, cried foul over the alleged transfer of Ksh.8.2 Billion museum project to Kajiado...

US lawmakers urge boycott of Saudi G20 summit

Members of the US Congress have called on the government to boycott the G20 summit being held in Saudi...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you