News Mgomo wa wafanyakazi wa umma Ugiriki

Mgomo wa wafanyakazi wa umma Ugiriki

-

 

Wafanyakazi wa umma wamefanya mgomo wa siku moja katika mji mkuu wa Athens nchini Ugiriki kwa ajili ya kupinga sera za serikali za uchumi na usalama.

Mgomo huo uliofanyika kufuatia wito wa Shirikisho la Wafanyikazi wa Umma wa Ugiriki (ADEDY) na Chama cha Waalimu (OLME), umeathiri vibaya maisha ya kila siku katika mji mkuu.

Wafanyakazi kutoka sekta ya usafiri wa umma na huduma ya afya pia walishiriki mgomo huo na kusababisha usitishaji wa huduma za metro, treni, mabasi na hospitali za serikali.

Kumekuwa na usumbufu wa safari za ndani na nje ya nchi kufuatia upanguaji wa ratiba za usafiri wa ndege uliosababisha na mgomo wa wafanyakazi wa shirika la usafiri wa anga (YPA).

Kwingineko, wanachama wa ADEDY, OLME na mashirika mengine, walikusanyika kwenye eneo la Klaftmonos Square ili kuandamana hadi kwenye eneo la Sintagma Square liloko karibu na jengo la bunge.

Maafisa wa polisi walioshambuliwa kwa vilipuzi vya chupa na kundi moja la waandamanaji, walikabiliana nao kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwakamata watu 10.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Coronavirus Immunity May Only Last A Few Months after Infection: Study

- Science news - Research by Imperial College London estimated just 4.4% of adults had some form of...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you