News Mwakamo aahidi kukomesha kero ya mifugo

Mwakamo aahidi kukomesha kero ya mifugo

-

 Na Omary Mngindo, Ruvu

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo amewahakikishia wakazi jimboni hapa kuwa, kero ya mifugo katika mashamba itabaki kuwa historia.

Amewataka wakulima kujiandaa katika kilimo na kwamba atahakikisha kero iliyopo ya mifugo kuingizwa katika mashamba itadhibitiwa, na kwamba atakachokifanya ni kusimamia utekelezwaji wa sheria zilizopo, ambazo wanaotakiwa kuzifuatilia ndio wanaosababisha tatizo hilo.

Mwakamo alitoa kauli hiyo akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ruvu kwa Dosa Azizi, akiomba kura za kutosha kwa John Magufuli, Ubunge kwa Mwakamo na Udiwani Godfrey Mwafulilwa, ambapo aliwaomba wananchi hao kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kuwachagua wana-CCM.

“Nakumbuka miaka iliyopita mkulima alikuwa analima mpunga, akivuna anapanda mahindi, miwa, maboga sanjali na mboga aina mbalimbali, ambapo kwa miaka ya hivi sasa jambo hilo halipo, sitotumia nguvu nitakwenda kupambana na wanaotakiwa kusimamia sheria ziliopo,” alisema Mwakamo huku akishangiliwa na wananchi.

Awali wazee wa Kijiji hicho wakiongozwa na Hemed Luwayo na Nuru Mshana waliwafanyia matambiko ya kimira Mwakamo na mgombea udiwani Mwafulilwa, yaliyolenga waombea dua katika safari yao hiyo, ili wachaguliwe sanjali na kutekeleza majukumu yao kea uadilifu mkubwa.

“Binafsi najisikia vibaya leo hii ninapowaona wazee wetu wakiangaika katika kujitafutia ridhiki kupitia kilimo, ambacho kwa miaka hii imekuwa mtihani mkubwa unaosababishwa na ndugu zetu wafugaji wanaovamia marnro yamashambani,” alisema Mwakamo.

“Leo hii wazazi wetu wanapolima mpaka kuvuna roho juu kutokana na baadhi ya wafugaji wasiozingatia utu kuingiza mifugo katika mashamba, hii inachangiwa na baadhi ya viongozi wenye mamlaka kushindwa kufuatilia sheria zinazowaongoza, ichagueni CCM nakwenda kumaliza kero hiyo,” alisema Mwakamo.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo kutoka mkoani Rugemalira Rutatina aliwataka wana-Ruvu kwa Dosa kuachana na ushabiki wa kisiasa, badala yake wakichague Chama Cha Mapinduzi ili chini ya Mgombea wa Urais Dkt. John Magufuli wakamizie kazi nzuri waliyoianza.

“Unapopita Ubungo na Tazara katika yake madaraja ya juu nafsi yako inakulazimisha Oktoba 28 kumchagua Dkt. John Magufuli, kutokana na kazi nzuri sanjali na utekelezaji wa miradi mikubwa inayoebdelea kutekelezwa kila kona hapa nchini,” alisema Rutatina.

Kwa upande wake mgombea udiwani Kata ya Mtambani Godfrey Mwafulilwa alisema kuwa katika Kijiji cha Ruvu kwa Dosa miaka mitano iliyopita kilikuwa na changamoto ya kukosekana kwa umeme na maji changamoto ambazo zimeshafanyiwakazi.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Cork-based solar energy company gets restraining order against winding up petition

A High Court injunction had been granted restraining the presentation of a winding up petition for a solar energy...

Manchester United’s revenue shrinks by almost 20% in last financial year

Manchester United’s revenue shrank by almost 20 per cent in the last financial year and the impact of Covid-19...

Passengers Stuck Inside Madaraka Express Train as Tremors Hit Voi

Passengers aboard the Madaraka Express train travelling from Mombasa to Nairobi were on Wednesday, October 21, stuck for an...

Simple Car Loan Saves Neighbourhood

I can still remember the day, Friday November 19, 2019. Something caught the corner of my eye while watching...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you