News Pompeo aikosowa Uturuki kwa kuhusika mzozo wa Nagorno-Karabakh

Pompeo aikosowa Uturuki kwa kuhusika mzozo wa Nagorno-Karabakh

-

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, amesema ushiriki wa Uturuki kwenye mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia, unaongeza hatari ya machafuko hayo kugeuka kuwa ya kikanda, akirejelea wito wake wa kuutatuwa mkwamo uliopo kwa njia ya mazungumzo.

 Mamia ya watu wameshauawa kwenye mapigano ya sasa katika jimbo la Nagorno-Karabakh, yanayotajwa kuwa mabaya kabisa tangu yale ya mwaka 1990, yaliyoangamiza maisha ya watu 30,000. Jimbo hilo ni sehemu ya Azerbaijan kwa mujibu wa sheria za kimataifa, lakini limekuwa likikaliwa na kutawaliwa na watu jamii ya Kiarmenia. 

Mapigano yaliyozuka mwanzoni mwa mwezi huu, yanahofiwa huenda yakazifanya Urusi, inayoiunga mkono Armenia, na Uturuki, inayoiunga mkono Azerbaijan, kuingia kwenye mvutano, kama inavyoshuhudiwa pia nchini Syria na Libya, ambako mataifa hayo yanaunga pia mkono pande tafauti.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you