News Rusesabagina 'aliandika barua' kutoka jela

Rusesabagina ‘aliandika barua’ kutoka jela

-

Vincent Lurquin, wakili Mbelgiji amesema alipokuwa mjini Kigali alipata barua kutoka kwaPaul Rusesabagina inayosema kuwa mawakili anaowataka ni wawili , ambao ni miongoni mwa mawakili saba waliopangwa na familia yake.

Mapema leo asubuhi ‘’shujaa huyo wa filamu yaHoteli Rwanda’’ alikataliwadhamana, na anashikiliwa katika gereza kuu la Kigali akisubiri kesi ya mashitaka ya ugaidi dhidiyake, ambayo hajayakubali bado.

Bw Rusesabagina ianasaidiwa na mawakili wawili wa Rwanda ambao waendesha mashitaka wa Rwandawalisema walichaguliwa na mshukiwa binafsi.

Katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika kwa njia ya video Alhamisimawakili wawili kati ya saba waliopangwa na familia yake waliwaambia waandishi wa habari kuwa walipokuwa Kigali walizuiwa kumuona Bw Rusesabagina.

Bw Lurquin alisema kuwa amekuwa wakili wa Bw Rusesababgina nchini Ubelgiji naalikuwa mjini Kigali kumuona mteja wake na kupata haki ya kumuwakilisha.

“ Kwa miaka miwili iliyopitaUbelgiji imekuwa ikichunguza kesi dhidi ya Bw Rusesabagina, na nimekuwa wakili wake tangu wakati huo” – Bw Lurquin alisema.

“Sioni ni kwanini Rwanda ilinizuwia kumuona na kumsaidia mteja wangu, raia wa Ubelgiji juu ya kesi ambayo ilianzia Ubelgiji.” Aliongeza.

Wakati alipokuwa Kigali Bw Lurquin alisema kuwa alipata barua kutoka gerezani iliyoandikwa na BwRusesabagina akiwakubali mawakili Gatera Gashabana, wakili anayeishi Rwanda Vincent Lurquin, kama mawakili aliowachagua binafsi kumuwakilisha katika kesi dhidi yake.

Amesema kuwa katika kipindi cha wiki mbili atarejea Rwanda na timu ya mawakili kushinikiza haki ya kumuwakilisha mteja wake.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Over 450,000 Patients Recover from COVID-19 in Iran

- Society/Culture news - Speaking at a daily press conference on Saturday, Sima Sadat Lari said at least...

San Bernardino Police Fatally Shoots Black Man (+Video)

- World news - The man, identified as Mark Matthew Bender Jr., 35, died at a local hospital,...

How Police Mistakenly Chauffeured CBK Governor’s Look-Alike to Nairobi CBD

Central Bank of Kenya Governor Patrick Njoroge has narrated how his lookalike kin was granted police escort in a...

Sudan Umma Party threatens transitional government over ties with Israel

The Sudanese Umma Party, led by Sadiq Al-Mahdi, on Thursday threatened the transitional government of his country over the normalisation...

Leader Urges Decisive Decisions, Collective Action to Tackle COVID-19 in Iran

- Politics news - Iranian President Hassan Rouhani and members of the Coronavirus Fight National Headquarters met with Ayatollah...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you