News Serikali yakutana na wazalishaji wa Saruji nchini

Serikali yakutana na wazalishaji wa Saruji nchini

-

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki  wamefanya kikao cha pamoja na wazalishaji wa saruji nchini kwa lengo la kujadili fursa mbalimbali, changamoto na namna bora ya kukuza sekta ya ujenzi nchini kupitia saruji, kikao kilichofanyika Ofisi za Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), jijini Dar es Salaam.  Leo 17.10.2020

Katika kikao hicho, Mawaziri hao wamekutana na kampuni 9 za saruji zikiwemo Dangote Cement, Camel Cement, Nyati Cement, Mbeya Cement, Kilimanjaro Cement, Maweni Cement, Tanga Cement, Lake Cement, Twiga Cement pamoja na Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI), wakijadili namna bora ya kuendeleza sekta hiyo.

Waziri Bashungwa aliwapongeza wazalishaji hao kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwasihi wasipandishe bei ya saruji kiholela hasa kuzingatia kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya 5 ni kuiona Tanzania inakua nchi ya viwanda.

Wazalishaji hao walizungumzia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo ubovu wa barabara hasa kipindi cha mvua, unaofanya bei kuwa juu kidogo, upatikanaji wa nishati madhubuti kama gesi, suala la kodi na kuiomba serikali sikivu kushughulikia changamoto hizo.

Nae, Waziri Kairuki alisema kuwa wizara yake na Wizara ya Viwanda wanafanya kazi kwa ukaribu na kuwatoa hofu wazalishaji hao wa saruji kuwa serikali ipo pamoja nao na inashughulikia changamoto zao na kuwahakikishia wizara yake yenye dhamana ya uwekezaji itahakikisha inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hao.

Nae Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa aliwahakikishia wazalishaji hao kuwa serikali ina angalia namna bora ya kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi hasa kwa viwanda vilivyopo Ukanda wa  Pwani pia amewahakikishia kuwa changamoto nyingine ndogo ndogo atazishughulikia ndani ya wiki moja ijayo.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Zendaya shares surprising Euphoria news

Zendaya has surprised fans by announcing two special episodes of Euphoria are on the way. The actress – who last...

UK exposes Russian cyber attacks against Tokyo Olympics

The Russian military intelligence service (GRU) carried out cyber attacks on officials and organisations linked to the 2020 Tokyo...

Pretty Woman boots and Top Gun bomber jacket up for auction

Tom Cruise’s Top Gun bomber jacket and Julia Roberts’ Pretty Woman boots are going under the hammer. More than 900...

Link found between air pollution and neurological disorders – study

A significant link has been found between air pollution and an increased risk of hospital admissions for neurological disorders...

Court says Epstein’s ex-girlfriend’s testimony can be public

A British socialite’s testimony in a lawsuit related to Jeffrey Epstein’s sexual abuse activities can be made public, an...

Mobile phones are killing us

Hugh Grant has dubbed mobile phones “toxic”, saying “they are killing us”. The film star, 60,  relished leaving his phone...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you