News Tanzania wanawake waongezeka vitambi (Vilibatumbo)

Tanzania wanawake waongezeka vitambi (Vilibatumbo)

-

 

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Naibu waziri wa kilimo Omary Mgumba ametoa wito kwa wanawake nchini kuzingatia kanuni baora za lishe na kufanya mazoezi ili kupunguza tatizo la vitambi linalozidi kukua kutokana na ulaji usiozingatia kanuni.

Mgumba ametoa wito huo mkoani Njombe kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe.

“Kwa upande wa akina mama unene umeendelea kuongezeka,Kina mama wameendelea kuongeza vilibatumbo kwasababu ya mlo usiozingatia kanuni bora na lishe” Alisema Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

 Aidha amesema“Nitoe wito kwa kina mama wote nchini,ni vizuri wakaongeza jitihada za kuzingatia mlo uliozingatia kanuni bora za lishe na waendelee kufanya mazoezi ili kupunguza vilibatumbo” Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

Vile vile amesema tatizo la udumavu kwa watoto limepungua nchini

 “Tathmini inaonyesha tumepunguza tatizo la udumavu kwa watoto chini ya miaka 5 kutoka 34% mwaka 2015 hadi 32% mwaka 2018.Lakini idadi ya waoto waliothirika na tatizo hili limeongezeka kutoka watoto milioni mia mbili nukta saba mwaka 2015 hadi kufikia watoto milioni tatu mwaka 2018”alisema Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

Katika swala la ukondefu kwa watoto amesema hali imezidi kuimarika “Ukondefu kwa watoto chini ya miaka mitano hali imeendelea kuimarika vizuri,kwani tumefikia 5% sawa na malengo yaliyoekwa tusizidi 5% ifikapo 2021” Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

Kutokana na mkoa wa Njombe kuwa na zualishaji mkubwa wa mazao ya chakula licha ya kukabiliwa na tatizo la udumavu,amesema serikali inaendelea kufanya jitihada kupanua soko la parachichi kwa kuwa kumekuwa na uzalishaji mkubwa wa zao hilo

“Serikali tumeendelea kufanya jitihada na wenzetu wa mkoa wa Njombe,kuendelea kufanya upanuzi wa soko la parachichi  na tuko kwenye hatua za mwisho kupata itifaki ya kibiashara na wenzetu wachina ambao ni soko kubwa duniani” Amesema Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

“Ninawasihi sana wananchi wa mkoa wa Njombe na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha tunazingati mlo kamili na ulaji bora hasa kwenye chakula cha watoto wetu na hususani wa chini ya miaka miwili” Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

Mgumba amesema “Serikali chini ya Dkt,John Pombe Magufuli tumeshatumia zaidi ya bilioni 94 kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji hapa nchini”

“Baada ya kuongeza tija na uzalishaji kwenye mazao ya kilimo,mifugo pamoja na uvuvi,tumeweza kufanikiwa sana kiuchumi na kudhibiti mfumuko wa bei kutoka 5.59 mwaka 2015 na leo kuwa na 3.86%  mwaka 2020” Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo

“Tathmini iliyofanyika hivi karibuni 2019-2020  inaonyesha uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka mpaka kufikia tani milioni kumi na saba,laki saba arobaini na mbili na mia tatu themanini na nane.Ukilinganisha na mahitaji yetu kwa mwaka ya tani milioni kumi na nne laki tatu arobaini na saba mia tisa na hamsini na tano” Omary Mgumba Naibu waziri wa kilimo.

Bruno Mwepelwa (BM green Garden) na Stiven Mlimbila (Names Green Garden) ni baadhi ya wakulima na waoteshaji wa parachichi waliofika katika maonesho hayo,wamesema mkoa wa Njombe una kila neema katika uzalishaji wa mazao ya Chakula hususani Parachichi wamesema wanaomba wananchi kuendelea kuzingatia mlo kamili ili kuendelea kukuza kilimo hicho.

“Sisi tunazalisha parachichi na kuotesha miche bora aina ya hasi vile vile tunaendelea kutoa elimu juu ya parachichi na kipato cha parachichi kwa kweli soko limetanuka duniani tunashindwa sisi”alisema Bruno Mwepelwa (BM green Garden)

Stiven Mlimbila alisema “Kwa kweli maonyesho haya ni makubwa na yana tija kwa kuwa yamekusanya watanzania wengi na ukiangalia zao hili tumeingiza kwenye zao mkakati kwa hiyo tunaamini za olitakuwa na tija na Mh,Rais alipokuja Njombe aliahidi kutusaidia ikiwemo ujenzi wa miundmbinu”alisema Stiven Mlimbila (Names Green Garden)

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Wananchi wa Chamwino Ikulu wajitokeza kwa wingi vituoni kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani

Wananchi wa Chamwino Ikulu mkoani Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kituo cha kupigia kura cha Ukumbi wa Kijiji...

Schools Reopening: Magoha Offered Solution on All Students’ Return

Health CS Mutahi Kagwe and his Education counterpart George Magoha have been offered a solution on how to ensure all...

DJ wa Harmonize afunguka mahusiano yake na Linah (+Video)

try{__scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress();}catch(e){setTimeout( function(){ __scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress(); } , 3000 )};DJ wa Harmonize maarufu kama DJSEVE @djsevenworldwide amefunguka mahusiano...

Job Opportunity at Yetu Microfinance Bank PLC, Branch Manager

 Position: Branch Manager Location: Mngeta, Kilombero District Key details Yetu Microfinance Bank...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you