News Trump na Biden wakabiliana katika mdahalo wakiwa vituo viwili...

Trump na Biden wakabiliana katika mdahalo wakiwa vituo viwili tofauti

-

 

Wagombea wakuu wa urais nchini Marekani, Donald Trump wa Republican na Joe Biden wa Democratic, wamejitokeza katika vituo viwili tofauti vya televisheni. 

Katika mdahalo huo kila mmoja amemtuhumu mwenzake, juu ya namna anavyouchukulia ugonjwa wa COVID-19, sambamba na siasa za ndani na za kimataifa. 

Kwa wengi, mahojiano hayo yamechukuliwa kama duru ya pili ya mdahalo wa uso kwa macho kati ya Trump na Biden, ambao awali ulikuwa umepangwa kufanyika jana, lakini Trump akajitowa baada ya waandaaji kuamuwa ufanyike kupitia mtandao, kufuatia Trump kuuguwa COVID-19 wiki mbili zilizopita.

 Akihojiwa na kituo cha televisheni cha ABC mjini Philadelphia, Biden alisema Trump hajayachukulia kwa umakini zaidi maradhi hayo, ambayo yashawaangamiza Wamarekani zaidi ya laki mbili.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Jimbo Katoliki la Sumbawanga lazindua jengo la Wagonjwa wa nje wa Macho

Katika kusaidia juhudi za serikali kuboresha huduma katika mkoa wa Rukwa, Jimbo Katoliki la Sumbawanga kwa ufadhili wa Shirika...

Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi aagiza wasimamizi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria

 Na Amiri Kilagalila,Njombe Mratibu wa uchaguzi mkoa wa Njombe bwana Hilmar Danda amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi za jimbo...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you