News Tundu Lissu aendelea na kampeni zake Singida

Tundu Lissu aendelea na kampeni zake Singida

-

 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,( CHADEMA) Tundu Lissu,amewataka wananchi kuchagua serikali itakayosimamia haki,uhuru na maendeleo ya watu.

Akizungumza hii leo Oktoba 11,2020,katika Kampeni zake zilizofanyika katika eneo la Iguguno Iramba Mashariki, Mkoani Singida, mgombea huyo amewataka wananchi hao kuacha kulalamika badala yake wachukue hatua ili waweze kupata maendeleo yenye maana kwao.

 ‘’Kama unataka kuwa huru  kuuza biashara  zako ukiwa huru,uuze chochote unachozalisha ukiwa huru chagua Tundu lissu’’amesema Tundu Lissu,

‘’Mtoto wako akienda shuleni au hospitali atendewe haki na sio kununua haki, mama lishe atendewe haki na bodaboda atendewe haki’’ameongeza Tundu Lissu

Aidha Lissu amesema kuwa hata kwenye maandiko Matakatifu yameandika  haki huinua taifa hivyo taifa  litainuka kukiwa na haki na tukiwa huru.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you