News “Ulaji wa nyama Tanzania hauridhishi” Dk,Rashid Tamatama

“Ulaji wa nyama Tanzania hauridhishi” Dk,Rashid Tamatama

-

 

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Licha ya nchi ya Tanzania kuongeza uzalishaji wa samaki katika sekta ya uvuvi pamoja na kuongezeka kwa mifugo katika sekta ya mifugo lakini bado ulaji wa nyama ili kutengeneza lishe kwa watanzania umekuwa sio wa kuridhisha.

Katibu mkuu wizara ya mifugo Uvuvi Dk,Rashid Tamatama amebainisha hayo maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe.

 

“Pamoja na ongezeko la uzalishaji wa zao la nyama bado ulaji wa nyama na maziwa nchini sio wa kuridhisha,niendelee kutoa rai kwa wananchi kuongeza ulaji wa Nyama ili tuweze kufikia kiwango kilichosimikwa na shirika la kilimo na chakula”Katibu mkuu wizara ya mifugo Uvuvi Dk,Rashid Tamatama

Vile vile amesema “Kila mtu inatakiwa ale angalau kilo 50 za nyama kwa mwaka,na kila mtu pia inatakiwa anagalau anywe lita 200 za maziwa kwa mwaka” Katibu mkuu wizara ya mifugo Uvuvi Dk,Rashid Tamatama

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Coronavirus Immunity May Only Last A Few Months after Infection: Study

- Science news - Research by Imperial College London estimated just 4.4% of adults had some form of...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you