News Urafiki umemuondoa Suarez Barcelona

Urafiki umemuondoa Suarez Barcelona

-

 

Aliyekuwa mshambuliaji wa FC Barcelona Luiz Suarez amesema klabu hiyo ilimuuza ilikumuweka mbali na rafiki yake Lionel Messi, kwa sababu aliunga mkono mawaza ya La pulga kuomba kuondoka klabu hapo.

Messi aliingia kwenye mgogoro mkubwa na bodi ya FC Barcelona baada ya kuomba kuondoka klabu hapo, lakini uongozi wa Barca ulikataa ombi hilo na sasa amesalia Camp Nou mpaka mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utamalizika.

Suarez amesema “Messi alitaka kuondoka na klabu haikutaka. nilijaribu kumsaidia na kumsumbua kidogo, Nadhani walitaka kuniondoa karibu na Messi, labda iliwasumbua kwamba nina mahusiano mazuri na Leo’’. Labda walitaka asiwe na mimi sana.’’

Licha ya kucheza kwa mafanikio Luiz Suarez hakuondoka vizuri Barcelona na inaripotiwa Rais wa Barcelona Josep Bartomeu alitaka kuzuia usajili wake wa kujiunga na Atletico Madrid.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 34 ameondoka Barcelona akiwa mfungaji bora namba tatu wa muda wote wa klabu hiyo akiwa na mabao 198 katika michezo 209 nyuma ya kinara Lionel Messi na Cesar.

Na ameshinda jumla ya mataji 13 akiwa na Barcelona, ukiwemo ubingwa wa ligi kuu Hispania La liga mara 4 na ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara 1.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

€4m Covid lab under construction at University Hospital Limerick

A €4million purpose-built Covid-19 laboratory, which will boost testing capacity at University Hospital Limerick (UHL) by 70 per cent,...

Obama kupanda jukwaani kumpigia debe Biden

 Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama anafanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara leo mjini Phidadelphia kumpigia debe...

Israel detains child in night raid in occupied West Bank

Israeli occupation forces arrested 14 Palestinians, including at least one child, in night raids across the occupied West Bank,...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you