News ''Vijiji vyote wilayani Ludewa kupatiwa umeme ''Wakili Joseph Kamonga

”Vijiji vyote wilayani Ludewa kupatiwa umeme ”Wakili Joseph Kamonga

-

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mbunge mteule jimbo la Ludewa CCM wakili msomi Joseph Kamonga ameendelea na Kampeni za kumuombea Kura Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Madiwani wa CCM Kwenye kata za wilaya ya Ludewa  kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 na tayari amekwisha tembelea kata 17.

Wakili Kamonga amewaeleza wana-Ludewa kuwa wanapaswa kukiamini Chama Cha Mapinduzi na Viongozi wake kama walivyomuamini yeye na kumpitisha bila kupingwa ”Ndugu zangu niwahakikishie kwa imani hii mliyoionyesha kwenye Chama cha Mapinduzi  na mimi binafsi , nawaahidi sitawaangusha nipo tayari kuwawakilisha mnitume muwezavyo kwani utumishi sio ubwana mkubwa ni kuwatumikia watu” amesema Wakili Kamonga

Katika hatua nyingine Mbunge Mteule  Joseph Kamonga alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara katika kata ya Ludende ameeleza kuwa zaidi ya bilioni 8 zimetumika katika miradi ya umeme wilayani Ludewa Mkoani Njombe ambapo bilioni 5 zimetumika kwenye umeme wa rea na bilioni 3 kwenye Umeme wa Gridi ya Taifa ambapo Vijiji 60 vilivyopo wilayani humo tayari vimepata umeme na kubakiwa na Vijiji 17.

“Najua kuwa umeme haujafika vitongoji vyote lakini kwa maelezo ya meneja wa Tannesco utafika kwenye vitongoji vyote vya Ludewa , jamani ni kazi kubwa sana ameifanya Rais Magufuli kwenye sekta ya umeme”. amesema Wakili Kamonga

Sanjari na suala hilo la Umeme Mbunge huyo amesema serikali bado inaendelea kuboresha Miundombinu ya Barabara zinazounganisha kata mbalimbali za wilayani humo , ikiwemo barabara inayoendelea kujengwa kutoka Itoni hadi Manda kiwango cha Zege , Pia Kutoka mkiu , Mundindi , Mavanga hadi Madaba kwa kiwango cha Lami na Kilomita 70 Kuunganisha Liganga na Mchuchuma na tayari upembuzi yakinifu umefanyika.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Wananchi wa Chamwino Ikulu wajitokeza kwa wingi vituoni kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani

Wananchi wa Chamwino Ikulu mkoani Dodoma wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kituo cha kupigia kura cha Ukumbi wa Kijiji...

Schools Reopening: Magoha Offered Solution on All Students’ Return

Health CS Mutahi Kagwe and his Education counterpart George Magoha have been offered a solution on how to ensure all...

DJ wa Harmonize afunguka mahusiano yake na Linah (+Video)

try{__scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress();}catch(e){setTimeout( function(){ __scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress(); } , 3000 )};DJ wa Harmonize maarufu kama DJSEVE @djsevenworldwide amefunguka mahusiano...

Job Opportunity at Yetu Microfinance Bank PLC, Branch Manager

 Position: Branch Manager Location: Mngeta, Kilombero District Key details Yetu Microfinance Bank...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you