News Vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kuhusu...

Vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kuhusu mauzo ya silaha vyafikia mwisho

-

Vikwazo ambavyo vimedumu kwa muongo mmoja vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kununua silaha kama vifaru na ndege za kivita vimefikia mwisho leo kama ulivyopangwa kulingana na mkataba wa Iran kuhusu silaha za nyuklia kati ya taifa hilo na nchi zenye nguvu zaidi duniani. 

Hiyo ni licha ya pingamizi kutoka Marekani. Kwenye ukurasa wake wa Twitter, wizara ya Mambo ya nje ya Iran imesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sasa inaweza kununua silaha zozote na zana nyinginezo kutoka nchi yoyote bila ya vikwazo, na itategemea tu mahitaji yake ya ulinzi. 

Rais wa Marekani Donald Trump aliiondoa nchi yake kwenye mkataba huo mnamo mwaka 2018. Lakini amekuwa akitaka vikwazo hivyo dhidi ya Iran virefushwe. Hata hivyo mnamo Agosti mwaka huu, Marekani ilishindwa kupata uungwaji mkono wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Njombe:TAKUKURU yawatamani viongozi wasioona aibu kukemea Rushwa

Na Amiri Kilagalila,NjombeTaasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Njombe,imetoa rai kwa wananchi kuchagua viongozi wapenda...

Amnesty: Waandamanaji 12 wauawa Nigeria

Lagos:Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema katika ripoti yake jana kwamba vikosi vya usalama...

Kenyan Vegetable Vendors Make Ksh235M in 3 Days Online

A group of Kenyan vegetable vendors raked in Ksh235 million over the last 3 days in an online virtual...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you