News Watu 31 wafariki kutokana na kimbunga Molave Vietnam

Watu 31 wafariki kutokana na kimbunga Molave Vietnam

-

Mchakato wa uokozi unaendelea nchini Vietnam hii leo, baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na KimbungaMolave. 

Mamia ya wanajeshi wenye vifaa vizito wametumwa katika maeneo ya ndani ya jimbo la Quang Nam kulikotokea maporomoko ya ardhi na ambako watu 19 wameuawa na wengine 48 hawajulikani walipo. 

Aidha miili ya wavuvi 12 imeopolewa baharini hii leo na wengine 14 hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama. 

Kimbunga hicho kinatajwa kuwa ni kibaya kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa. Na kimepiga katikati mwa nchi, ambako tayari kumekuwa kukinyesha mvua kali kwa wiki kadhaa zilizosababisha vifo vya watu wapatao 160. 

Zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na dhoruba hizo kali ziliozopiga kwa wiki kadhaa. Mashirika ya kutoa misaada nayo yameelemewa kutokana na idadi kubwa ya walioathirika.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

North preparing for Covid-19 vaccine rollout from next month

Preparations are well under way to begin the rollout of a Covid-19 vaccination programme from next month in Northern...

Mamilioni ya Wamarekani wasafiri licha ya maonyo ya maambukizi ya covid

Mamilioni ya watu nchini Marekani wanasafiri kabla ya likizo ya siku ya Shukrani, licha ya kuongezeka kwa idadi ya...

Americans travel home for Thanksgiving despite coronavirus surge

Millions of Americans took to the skies and the roads ahead of Thanksgiving at the risk of pouring petrol...

UN decries police use of racial profiling derived from ‘big data’

Police and border guards must combat racial profiling and ensure that their use of "big data" collected via artificial...

Last orders for Dublin’s Rí-Rá nightclub and The Globe bar

It’s ‘last orders’ for well known Dublin night venues, Rí-Rá nightclub and The Globe bar. Dublin City Council has approved...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you