News Zitto atangaza kumpigia kura ya Urais Tundu Lissu

Zitto atangaza kumpigia kura ya Urais Tundu Lissu

-

 

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema kuwa siku ya kupiga kura, atampigia kura mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu, kwa kuwa anamuamini sana na anayo dhamira ya dhati kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Oktoba 16, 2020, na Kiongozi huyo na kusema kuwa chama hicho kimeshauriana na kuona kuwa kuna haja ya kuchagua kiongozi ambaye atarejesha furaha na kuheshimu katiba ya nchi.

“Kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi nitapiga kura yangu kwa ndugu Tundu Lissu, huyu ndiye mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda mgombea wa chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo”, amesema Lissu.

Aidha Zitto amewaomba Watanzania kwa pamoja wampigie kura Lissu na kusema kuwa, “Sisi ACT Wazalendo hatupo tayari kuwa kizuizi cha safari hii ya mabadiliko, nami kama kiongozi wa chama ninao wajibu wa kulieleza hilo kwa uwazi kwa niaba ya viongozi wenzangu wa kamati ya uongozi”.

Mbali na hayo Zitto amewataka Watanzania kuwachagua wagombea wa ACT Wazalendo katika majimbo na wagombea wa upinzani wenye nguvu zaidi, huku yeye akitoa msimamo wake thabiti juu ya mgombea gani atakayempigia kura.

Awali Chama cha ACT-Wazalendo kilimteua Benard Membe ambaye alipitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwania kinyang’anyiro cha urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Churchill Comedian Butita in Legal Battle With Global Firm

Popular comedian Edwin Butita popularly known as Eddie Butita on Thursday, October 22, initiated legal action against a global...

Europe’s Daily Coronavirus Cases Double in Ten Days

- World news - The continent first reported 100,000 cases in a day on October 12, although the...

Syria: Mufti of Damascus assassinated in car bombing

Sheikh Muhammad Adnan Al-Afiouni, the senior Sunni Muslimsy province was killed in a roadside bombing yesterday which is believed...

Irish Police Clash with Anti-Lockdown Protesters in Dublin (+Video)

- World news - Nine of the people arrested have been charged with public order offenses, as the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you