News Zuberi Katwila ajiuzulu ukocha Mtibwa Sugar

Zuberi Katwila ajiuzulu ukocha Mtibwa Sugar

-

Uongozi wa Mtibwa Sugar umethibitisha kuwa kocha Zuberi Katwila, amejiuzulu nafasi yake kuanzia leo Oktoba 18, 2020 baada ya kuwasilisha barua.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Sheria na Utawala, Sabri Aboubakar amesema uamuzi wa Zuberi kuondoka klabuni hapo ni wake binafsi na wao kama uongozi wamebariki baada ya pande zote mbili kuridhia.

Sababu za kujiuzulu kwa kocha huyo hazijawekwa wazi kufuatia makubaliano ya pande hizo mbili kukubaliana kuwa ni siri.

Katwila amejiuzulu ikiwa ni siku chache baada ya Mtibwa kupoteza mchezo wa tatu mfululizo wa ligi kuu na mara ya mwisho walinyukwa 2-0 na Gwambina.

Katwila amedumu katika klabu ya Mtibwa tangu mwaka 1999 akiwa mchezaji kabla ya kugeukia ukocha kwa miaka 8, huku mitatu katika hiyo alikua kocha mkuu wa wakatamiwa hao.

Mikoba yake kwa sasa imeachwa kwa Vicent Barnabas ambaye alikua msaidizi wake tangu kuanza kwa msimu.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Tunisia lets regions impose counter-pandemic curfews

Tunisia’s Prime Minister Hichem Mechichi on Monday gave regional governors the power to order curfews starting from Tuesday to...

Dundalk one step closer to European football after win against Derry City

Derry City 1 - 2 Dundalk Dundalk are a win away from securing an eighth consecutive season of European football. First-half goals from Sean Murray...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you