News Bajeti ya EU na mpango wa uokozi uchumi bado...

Bajeti ya EU na mpango wa uokozi uchumi bado kizungumkuti

-

 

Afisa mkuu anayehusika na uchumi katika Tume ya Umoja wa Ulaya Paolo Gentiloni, amezihimiza nchi wanachama kuunga mkono bajeti ya euro bilioni 1.8 na mpango wa uokozi wa janga la virusi vya corona, baada ya Hungary na Poland kuzuia uidhinishwaji wake. 

Gentiloni amesema nchi wanachama zinapaswa kuonyesha dhamira ya uwajibikaji kwa raia wao katika wakati huu mgumu. Siku ya Jumatatu Hungary na Poland zilizuia uidhinishwaji wa mpango wa uokozi na bajeti ya mwaka 2021-2027 kuhusiana na mvutano juu ya utawala wa sheria. 

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema Umoja wa Ulaya unataka kuhusisha masuala hayo na nchi kuheshimu utawala wa sheria, ili kuilazimisha nchi yake kukubali wahamiaji. 

Ujerumani inayoshikilia urais wa kupokezana wa Umoja huo, imeapa kuyashawishi mataifa hayo mawili kuondoa zuio hilo katika mkutano wa kilele utakaofanyika kesho.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Pandemic unemployment payment extended until March for ‘peace of mind’

The decision to extend the Pandemic Unemployment Payment (PUP) to the end of March is intended to give people...

Key witness who failed to give evidence in Aaron Brady trial jailed

A key witness failed to give evidence in the trial of Aaron Brady for the murder of Detective Garda...

Biden appoints first Palestinian-American to serve as a White House staffer

US President-elect Joe Biden appointed a longtime Palestinian-American Capitol Hill aide as the deputy director of the White House Office of...

Taharuki ya covid-19 nchini China

Hali ya taharuki imetanda kwenye uwanja wa ndege baada ya wafanyakazi wawili kukutwa na virusi vya corona (Covid-19) katika...

Mpyagila akaribia kukalia kiti cha uenyekiti wa halmashauri ya Nachingwea

Ahmad Mmow, Nachingwea.  Madiwani wa teule 40 wanaopitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, mkoani...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you