News BFA yavihimiza vilabu vyake kujisajili kwa Msajili

BFA yavihimiza vilabu vyake kujisajili kwa Msajili

-

Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

UONGOZI wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani (BFA), umevitaka vilabu wilayani hapa kuanza utaratibu wa kujisajili kwa Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo.

Hatua hiyo inalenga kuviwezesha kushiriki Ligi inayoandaliwa na chama hicho, sanjali na ligi nyingine kuanzia Daraja la Tatu ngazi ya Mkoa, la pili ngazi ya Taifa ikiwemo ya la kwanza zinazosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.

Hayo yameelezwa na Katibu wa BFA Salum Kanema akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa, ambapo alisema uongozi mpya uliochaguliwa Novemba 15 umedhamiria kuhamasisha vilabu kufuata sheria na taratibu za uendeshaji wa vilabu vyao.

“Tumeshaanza kazi ya kuwatumikia wanamichezo wa Bagamoyo, tunahakikisha mpira unachezwa kwa faida ya wana-Bagamoyo, tunatekeleza malengo ya kuviendelea vilabu vyote vikiwemo ambavyo bado havijasajiliwa na Msajili, ili visajiliwe hatimae kushiriki ligi hizo,” alisema Kanema.

Aidha amevitaka vilabu ambavyo vimeshasajiliwa na Msajili huyo, viwasiliane na uongozi wa BFA kwa lengo la kuweka vizuri taratibu zitakazowezesha kuboreshwa kwa mchezo huo wilayani hapa, ikiwemo kupanga mikakati mbalimbali ya kuanzisha mashindano.

“Bagamoyo tuna vilabu vingi, mfano Jimbo la Bagamoyo kuna timu si chini ya 43 ambavyo ni Mlingotini Fc, Pande Fc, Zinga kwa Mtoro, Zinga kwa Hawadhi, Kerege Fc, Kerege Academy, Kerege United (CCM), Mapinga Fc, Kiromo Fc, Makondeko United, Buma Fc, Kitopeni Fc, Ukuni Fc, Kaole Sc na Friends Fc,” alisema Kanema.

Nyingine Bagamoyo Veteran, Dunda United, Mwambao Fc, Mange Town, Masoko Fc, National Housing Fc, Salamanda Sc, Coast Star, Stand Fc, Mzalendo Fc (Buma), Young Star (Miswe), Sunguvuni Rangers, Matimbwa United, Buma Fc na Karavani Fc.

“Vingine ni Nianjema Sc, Zimbabwe United, Majengo Fc, Matikiti Fc, KLPT Sc, Saadan Fc, Macco Sc, Bongololo Fc, Nyongolota Fc, Makurunge Fc (Mkwajuni), Mkwajuni United, Fukayosi Fc na Mwavi Sc,” alisema Kanema.

Alisema kuwa vilabu vingi vinashiriki ligi zinazoanzishwa na Wadau, pasipokucheza ligi ya BFA, huku akiwaomba viongozi wa vilabu ukanda wa Jimbo la Chalinze kuwasilisha majina ya vilabu vyao kwa lengo la kuvibaini vilivyosajiliwa na Msajili na ambavyo bado ili utaratibu huo uanze.

 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Iraqi Min terms Iran, Iraq academic relations fruitful

TEHRAN, Dec. 06 (MNA) – The Iraqi Minister of Higher Education described the bilateral cooperation between the two neighboring...

“Equality, Sincere Assistance Maneuver” in Tehran

TEHRAN, Dec. 05 (MNA) – The 6th edition of “Equality, Sincere Assistance Maneuver” was held at Saheb al-Zaman (PBUH)...

Space-mad boy surprised by astronaut Chris Hadfield on Late Late Show

A six-year-old space enthusiast who warmed Irish hearts with his appearance on national television got a Christmas gift of...

‘Official’ Wife Blasts MP Murunga’s Lover During Burial

The late Matungu MP Justus Matungu's first wife Christabel Murunga addressed the parliamentarian's alleged lover Agnes Wangui Wambiri during the funeral...

Police mount cross-border operation targeting criminals and drink-drivers

Police in Northern Ireland and the Republic are carrying out a cross-border operation targeting criminals and drink-drivers over the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you