News Bob Wine kurejea kwenye kampeni zake Jumatatu

Bob Wine kurejea kwenye kampeni zake Jumatatu

-

Mgombea urais nchini Uganda wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi Ssentamu ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine atarejelea shughuli zake za kampeni Jumatatu.

Kampeni za Bobi Wine zilikatizwa Jumatano baada ya kukamatwa katika eneo la Luuka na kupelekwa kituo cha polisi cha Nalufenya. 

Katika ujumbe aliouweka hii leo kwenye mtandao wa Twitter, Bobi Wine ameashiria kutokata tamaa ya kile anachotaka kufikia.

Kwa mujibu wa msemaji wa chama chake cha NUP Joel Ssenyonyi, Bobi Wine atarejelea kampeni zake Jumatatu 23, Novemba katika eneo la Kyenjojo na Fort portal. 

Pia inasemekana kwamba kuna mipango ya kupanga tena kampeni katika maeneo alikotakiwa kufika kabla ya kukamatwa. 

Baada ya kuchiwa huru, Bobi Wine alisema wafuasi wake wamejitolea kuendelea kupigania mabadiliko nchini humo na kuongeza kuwa hatua ya kuongezwa kwa maafisa wa usalama ni ishara ya uoga, hofu na ukosefu wa matumiani.

Bobi Wine alifanya maombi maalum na kutuma rambi rambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao wakati wa vurugu zilizotokea wiki jana baada ya kukamatwa kwake.

Jumamosi asubuhi, magari ya vikosi vya usalama yaliegeshwa katika maeneo tofauti mjini Kampala huku polisi wakishika doria katika maeneo karibu na makao makuu ya chama cha upinzani cha People’s Power.

Polisi imetangaza kuwa ni watu 28 waliofarika katika maandamano ya siku ya Jumatano na Alhamisi, japo vyombo vya habari nchini Uganda vinanukuu vyanzo vya hospitali kuu kwamba idadi ya waliofariki ni watu 37.

Bobi Wine aliachiwa kwa dhamana siku ya Ijumaa, baada ya kushtakiwa kwa kukiuka kanuni za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka saba gerezani akipatikana na makosa. 

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

Permission for €500m wastewater treatment plant must be overturned, High Court rules

A High Court judge has ruled planning permission must be quashed for a proposed €500 million wastewater treatment plant...

21 Couples Tie the Knot in Mass Wedding [VIDEO]

A rare spectacle was witnessed in Merewet, Uasin Gishu after 21 couples made their vows at a go in a mass...

New host announced for 2021 edition of Grammy Awards

The Daily Show host and comedian Trevor Noah has been selected to host the 2021 Grammy Awards. The Recording Academy...

Ester Bulaya aapishwa kuwa Mbunge wa Viti maalum wa CHADEMA

Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya ameapishwa kuwa Mbunge wa Viti maalum wa ( CHADEMA). Mbunge...

Walioisababishia hasara TCRA wahukumiwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imewahukumu watu wawili kwenda jela miaka miwili au kulipa faini...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you